THAMANI YA MWANAMKE NI NINI:

Image result for love in africa

MWANAMKE, akilala na hali mumewe amemkasirikia, basi hulaaniwa na Malaika usikukucha.
Lakini sikujuwa kua kuna na kinyume chake.
Ilitokea katika khutba ya Ijumaa, lilitokea jambo ambalo si lakawaida, jamaa mmoja alimshitaki mkewe kwa Shekhe wa msikiti mbele ya watu.. SHEKHE akamjibu kua mwanamke hubeba jukumu kubwa la nyumbani kwake... na kuyavumilia mambo mengi kumshinda mwanamume, kwa mara zaidi ya mia na mia, na hata lau angekua huyo mwanamume ana misiba au matatizo mengi na akasubiri, lakini subira za mwanamke ni kubwa zaidi.. HAPO hata sauti ya huyo Shekhe ilianza kubadilika alipokuwa anamsemesha huyo mwanamume alomshitaki mkewe na kumwambia:
Mkeo amebeba mambo yako na ya watoto wako, na anasimama kwa miguu yake kuwatengezea chakula chenu. Na Mtume (s.a.w.) ameshausia hivo.. Jee kwani hana haki yeye ya kuheshimiwa? Na ya kuthaminiwa? Bila ya kumpunguzia chakula au kitu chochote anacho kihitaji?

BASI naapa Wallahi lau mwanamume anamkasirisha mkewe, akamgeukia na kumpa kichogo akatoka nyumba kumwacha mkewe na huzuni, basi Mwenyezi-Mungu anamlaani kwa kila khatwa anapokwenda, na kumyimia rizki yake, na kumpunguzia afiya yake, na kumuandikia kwa kila chozi moja linalotoka machoni mwa mkewake huyo.. makaa ya moto elfu moja kila siku, nusu yake duniyani, na nusu kesho akheera.. NATAMANI maneno haya yawafikie wanaume wengi walokwisha owa...
Machozi mangapi mengi yashamtoka mke wako na wewe hata hujali kabisa, wala huna hamu ya kitu chochote, wala hutaki kujua habari yake..
Musiyawache maneno haya kubakia moyoni mwenu tu, bali kila mtu awatumie walokwisha owa. Na ambao hawaja owa wahifadhi maneno haya msitari msitari kama akiba ya kesho yake watakapo owa.. AMESEMA Amiir Talaal Ar-Rashiid, Mungu amrehemu,:
(( Kama aliumbwa mwanamke kuwa ndege angekuwa ni "Tausi", na kama aliumbwa kuwa mnyama angekuwa ni "Paa" (Ghazala), na kama aliumbwa kuwa mdudu angekuwa ni "Kipepeo" (Butterfly), lakini ameumbwa kuwa mtu, kwa hivo yeye ndiye Mpenzi, na ndiye Mke, na ndiye Mama bora, na ndiye Neema nzuri kabisa ya mwanamume katika duniya hii..

Chapisha Maoni

0 Maoni