NITAMJUAJE MPENZI MDANGANYIFU...


NITAMJUAJE MPENZI MDANGANYIFU...
Kwanza napenda kuwapa pole wale wote ambao wanakumbwa na mikasa ya mapenzi.
Usijilaumu sana na kuona huna bahati ya kupendwa au kupata mapenzi ya dhati.
Somo letu la leo ni somo ambalo ni muhimu sana kwako wewe na ningependa ulitie maanani kwani ndilo litakalokusaidia kupata mapenzi ya dhati.
Watu wengi wamekuwa wakijiuliza ni jinsi gani wanaweza kuwatambua wapenzi wadanganyifu.
Nataka nikuambie kwamba huwezi kumtambua mwenzio vizuri kama mtakuwa hamjawa katika mahusiano. Hivyo somo hili linalenga zaidi kwa wale ambao tayari wako katika mahusiano.
Ni ukweli usiopingika kwamba,mtu anapokuwa anatafuta kitu huwa ni mpole na mkarimu. Ndio sababu inayomfanya kuaminiwa na kupewa kile alichokuwa anakihitaji.
Lakini baada ya kupata alichokuwa anakitaka ndipo anapoonyesha makucha yake.
Linapokuja suala la mahusiano,yakupasa uwe makini sana katika uchunguzi wa jambo hili. Usikurupuke kwani hutapata majibu.
Hizi ni baadhi ya ishara ambazo utaziona kama mpenzi wako ni mdanganyifu.
1: TABIA YAKE NA SAMAHANI ZISIZO ZA MAANA.
-Hakika kitu cha kwanza ambacho kitakuonyesha ni mabadiliko ya tabia yake. Hapo awali alikuwa akiomba umuandalie nguo za kuvaa,alikuwa anawahi kurudi nyumbani sasa anachelewa na unapomuuliza anakuwa mwepesi wa kuomba samahani,ambazo ni kama za kukuridhisha.
Muda wa kuwa karibu nawe unapungua,anakuwa busy kupita kiasi. Usikivu wake kwako unapotea,muda wote anakutuhumu wewe tu.
2: ATAANZA KUFICHA SIRI ZAKE.
-Hapo awali alikuwa akikushirikisha karibia kila kitu ambacho anakifanya au anatarajia kukifanya. Lakini taratibu utaanza kuona mabadiliko kwa mfano:
(a) Hatakuruhusu kupokea,kushika au kusoma meseji kwenye simu yake.
(b) Kama ana kompyuta atafuta mambo yote hasa yale aliyokuwa akiandika kuhusu mahusiano yenu.
(c)Atabadilisha namba ya simu,email.
(d) Anapopigiwa simu kama uko nae, atakuwa na wasiwasi na uongo utajengeka hapo.
3: KUKUTAMBULISHA NDUGU USIOWAJUA.
-Nina uhakika kwamba mnapokuwa kwenye mahusiano,ni lazima utawafahamu ndugu baadhi wa mpenzi wako.
Hata kama wengine wako mbali atakujulisha.
Lakini hali inapofikia hapa, utatambulishwa ndugu wasiokuwa na idadi. Na utakapotaka kufahamu zaidi kuhusu ndugu hao,anakuwa mkali.
Dalili hizi zinatosha kukuonyesha kwamba mpenzi wako ni mdanganyifu.

Chapisha Maoni

0 Maoni