MAPENZI YA KWELI YAPO? Kabla hatujajiuliza kama mapenzi ya kweli yapo inatupasa tujiulize na kufahamu neno "PENZI LA KWELI" ni nini? picha ambayo huwajia wengi vichwani mwao wanaposikia neno hili penzi la kweli huona kuwa ni watu wawili kupendana hata ikafikia hatua ya mmoja kugharamika roho yake kwa ajili ya faida ya mtu mwingine. Kama vile Romeo na Jullieth. Mapenzi ya kweli yapo na kuhakikishia ukiwa mvumilivu na kuacha hasira zako pembeni kesho nitawaeleza njia ya kulifanya penzi lako liwe la kweli ila leo tumalize siku kwa kutambua kama mwenzi wako ana penzi la kweli? 1 Haupo tayari kumpoteza. Wasichna wengi hawapo ayari kupoteza mahusiano yao. Hawapo tayari kuachana na mpenzi wake hata kama anafahamu mpenzi wake ana mahusiano na mwanamke mwingine atapigania penzi lake mpaka mwisho. 2 kuwa tayari kufanya mambo ambayo hayapendi kukuridhisha. Yupo tayari kwenda sehemu asiyoipenda kufanya mambo ambayo hajawahi kufanya ili wewe ufurahi na kulilinda penzi lake. 3 Nusu ya maisha yake atakupa wewe. Hii utaona pale ambapo ataacha mambo mengi kwa ajili yako kama alikuwa na ratiba za kujirusha na kufanya mambo yake jabla hajawa na wewe lakini akikuenda kweli atavunja nusu atakukabidhi wewe nusu atabaki nayo katika nzima ya uzima wake 4 yupo tayari kuangamia kwa ajili yako. Wengine hutamani hata kujiua au kufanya mambo ambayo yanahtarisha maisha yake ili ufahamu kuwa anakupenda hii hutokea pale ambapo unaenda kinyume na anavyotarajia. 5 kuwa tayari kuweka wazi ni kiasi gani anakupenda. Hatoogopa kuonekana malaya au ana tabia mbaya kwa watu wengine au kwako yeye anachojali kutimiza furaha ya nafsi yake. Hatokubali kunyamaza mpaka akuambie anakupenda kama ataona unachelewa (usisahau kulike page ile somo lijalo lisikupite) share kama umependa
0 Maoni