Hembu jibu meseji ya huyo dada, si mpenzi wako, mchumba na hata mkeo, anakutumia meseji asubuhi unaiona unakuja kusjibu usiku. Tena kakuuliza umeamkaje badala hata ya kumuambia vizuri uakataka kujua na hali yake unajibu “K” au “Ok” kama unajibu punda.
Kwani unapungukiwa nini ukijibu vizuri, au ndiyo ili na wewe utambe kuwa nakupenda sana kachanganyikiwa haishi kukutafuta. Kutwa zima anapiga simu kukujulia hali lakini wewe wala hata kupiga kuuliza alikuambia anaumwa anaendeleaje hupigi? Unajifanya uko bize kwa kazi ipi hasa ya kukufanya uko bize wakati u Desk Officer sehemu ni kupiga strori tu!
Kama uko bize unafanya nini kwenye magroup ya Whatsapp. Mwanaume mzima uneand akujadili Sijui Diamond, sijui Wema katembea na nani? Unatukana na povu kabisa lakini hata kulike picha ya mpenzi wako hutaki unaacha wanaume wenzako wanasifia.
Mtu ni Admin wa magroup saba ya Whatsapp halafu uanjifanya uko bize hata mkeo huwezi kujibu meseji yake moja. Badilika bwana ngoja sasa apate mtu wa kulike picha zake na kujibu SMS zake tuone kama magoli ya Ronaldo na Messi huko ulaya yatakusaidia kurudisha ndoa yako.
Hata kama kweli anakera anatuma meseji mia, hembu mjibu hata moja kistaarabu acha kumuumiza huyu binti wa watu. Anafanya yote hayo kwakua anakupenda, acha kumchukulia poa na kuumiza moyo wake kwa kitu kidogo kama kujibu SMS na kupokea simu, hembu mpigie nayeye ajisikie mwanamke!
Mtu mwenyewe kaamua tu kukuvumilia na shida zako sio kama una vigezo alivyokua anavitaka lakini unavyojishaua sasa, unataka unyenyekeweee kana kwamba umemhonga Bahari au una kiwanda cha pumzi kana kwamba hawezi pata kama wewe wakati mwenyewe matoleo ya zamani! Acha ushamba jibu meseji!
0 Maoni