Amewaacha wengine midomo wazi

Amewaacha wengine midomo wazi Jamaa huyo mwenye suti ya blue kwa jina la Uzor ambaye alioa January mwaka huu, amejitosa kutoa ushauri kuwa ni dhambi hasa kwa wakiristo hairuhusiwi mwanaume na mwanamke kutoa sauti za kimahaba wanapokuwa katikati ya tendo la ndoa kuashiria kunogewa na tendo hilo.
Amesema hata yeye alimpeleka mkewe huyo Kwenye maombi aache kabisa sauti hizo na sasa hazitoi tena zaidi ya hum hymns
Kupitia Facebook Jamaa huyo ameongeza kuwa mwanamke anayetoa sauti hizo Wakati wa tendo la ndoa ni ishara kuwa hana maadili au mwenendo mzuri na kwa mwanaume kutoa sauti za mahaba wakati wa tendo la ndoa ni ishara kuwa mwanaume huyo amejifunza mambo hayo kwa machangudoa
Anasisitiza kuwa, wakati wa tendo la ndoa mtu yeyote akitoa sauti hizo huku akitaja jina la Mungu au Jesus basi mtu huyo afungwe jela akieleza kuwa watu wanaomjua Mungu hawawezi kuvuka mipaka wala kutoa sauti hizo wakati wa tendo la ndoa.

Chapisha Maoni

0 Maoni