Wanaume Nisikilizeni dada yenu

Image result for warembo

Siku zote mwanamke ataishi na wewe kulingana na vile ambavyo unaishi nae. Ukiishi na mwanamke kwa furaha, upendo na amani, basi bila shaka mke atahakikisha analipa fadhila kwa kukupa furaha, upendo na amani ya moyo wako.

Ukiishi na mwanamke kwa heshima, huruma, na maelewano ndani ya nyumba, mwanamke hatokuwa na sababu ya kutokukuheshimu badala yake atafanya mara mbili ya wema unaomtendea.

Dhamana ya moyo wa mwanamke hujengwa kwa matendo mema ya mumewe, hivyo usijidanganye hata kidogo kuwa mke anaongozwa kwa sheria, ubabe na amri za kijeshi.

Mke huongozwa kwa upendo, upole pamoja na kumjenga kisaiklojia ili ajijue kuwa yeye ni mke na zaidi ya yote, yeye ni Mama.

Vile ambavyo utamtendea wema mke wako, ndivyo hivyo moto wa mapenzi unawaka katika moyo wake na kuzidisha ujuzi wa kuishi na wewe kwa upendo zaidi unaompa.

Brothers ishini na wake zenu kwa akili.
Nimemaliza

Chapisha Maoni

0 Maoni