Usife moyo kwa kupitia magumu Bali jipe moyo kuwa nitashinda

Related image

Daima kwenye maisha Kuna mengi magumu na mepesi siku moja nikiwa 4m 2 niliumia mguu kipindi Cha masika mama yangu alikuwa anaishi mjin Mimi kijijin ambako nilikuwa nasoma Basi baada ya kuumia mguu Kuna rafiki yangu alinisaidia Sana kupata watu wa kunipeleka hospital kushona baada ya kushona kile kidonda doctor aliniambia nisikanyage ili maji yasiingie kwenye jeraha
Basi nilikuwa naishi na mke wa mjomba ambaye ndie alikuwa karibu kwa wakati huo Basi baba mdogo alimfuata baba kuwa mtoto kaumia baba alisema Hana time nami na Wala hataki kusikia habari zangu
Nikiwa nauguza kidonda mke wa mjomba alikuwa hanijali kwa chakula Wala hata maji ya kuoga nikiwaomba watoto wake wakanipatie maji alisema nisiwasumbue watoto wake
Niliumia sana nililia Sana moyon mwangu kuwa ewe kifo kwann uchukue Kaka zangu na mdogo wangu pengine angenisaidia kupata hata mhindi wa kula
Basi ilinilazimu kwenda kutafta chakula baadae maji yakaingia ndan ya kidonda na kidonda kikaanza kuingiza wadudu Basi mguu wangu ukaanza kuoza mdogo mdogo baada ya siku 7 nilifungua kidonda na kuona unyayo wote umeoza hakika nililia Sana
Nilipelekwa hospital nikaambiwa inatakiwa mguu kutolewa hakika niliumia sana mama yangu aliposikia alikuja haraka sana na kuniambia kwann sijampigia simu kuwa niliumia
Daima sikusema chochote uchungu wa mwana aujue ni mama mama yangu alilia Sana hakika niliumia kwa maneno yake
Niliwambia kuwa Kama ni kufa Bora nife kuliko kubaki na nusu mguu kweli nilirudi nyumban na kuuguza mguu wangu na kupona kabisa baada ya kupona sikuamin macho yangu
Basi maisha yakazidi kusonga nikitafakari mengi lakin maswali mengi yalikuwa hayana majibu kamili
Ndugu yangu yawezekana unapitia wakati mgumu sana kwenye maisha kwenye ndoa yako au mahusiano yako au Kazin kwako daima naomba kukutia moyo kuwa
Hakuna safari ambayo Ina mafanikio ikose majaribu siku zote unapopitia magumu jua Mungu anakusudi na maisha yako
Pengine mmeo alikutelekezea watoto au mzaz mwenzio pengine mkeo mlevi na kahaba
Pengine wewe ni yatima unanyanyasika na baba wa kambo au mama wa kambo USIFE MOYO
#MadamKasema
Usife moyo

Chapisha Maoni

0 Maoni