Nilopoke tena sikiliza
Mwanamke anaweza kumpenda mwanaume anayempa pesa lakini mwanaume hawezi kumpenda mwanamke anayempa pesa. Moja ya vitu ambavyo vinatia aibu kwa mwanaume ni kuhongwa na mwanamke, wanaume wote unaoona wanalelewa mjini wapo wapo tu, hawapendi hiyo hali ila wanavumilia kwasababu ya shida na kupenda vyabure. Mhuwezi kumkuta mwanaume amekaa na wanaume wenzake anajisifia, “Mimi mke wangu ananinunulia nguo, ananilisha, amewasomesha wadogo zangu na sasa hivi ananijengea mimi napendwa!” Sijawahi kusikia, kwamba hata kama mwanaume anafanyiwa hivyo na mwanamke wake lakini kamwe, narudia kamwe huwezi kusikia anajisifia upuuzi huo na hata akijisifia wanaume wenzake watamcheka na kumuambia “Acha ufala wewe utaolewa watu watakuja kula Biriani!” narudia ni ngumu sana tena hata kama anaendesha Gari la mke wake au mwanamke wake basi atajificha na kama ni mbwembwe ataenda kuzionyeshea sehemu ambayo hajulikani, anahongwa Sinza anenda kula Bata Mbagala!
Ndiyo ilivyo kwa wanaume ni UFALA kuhongwa. Lakini vuta picha mwanamke anajengewa, kanunuliwa gari, anasomeshewa wadogo zake na anapewa kila kitu. Atakavyojishaua hata Kumbikumbi wataona wivu. Mwanamke anasikia raha kupewa pesa na mwanaume, anafurahia na anaweza kumpenda mwanaume, tena sana kwakua anahonga anahudumia. Ila narudia Mwanaume! Mwanaume hawezi kumpenda mwanamke kwakua anamhonga, tena watu wakijua mwanaume ataona hata aibu kuongozana na huyo mwanamke hata kama ni mkewe.
Hatajisikia raha, atajiona kama Dereva tu kumuendesha mwanamke ambaye amemhonga gari. Ndiyo maana nasema kuwa mwanamke ukishaona unaanza kumhonga mwanaume ili akupende basi jua kuwa ishakula kwako. Ni kama umempaka huyo mwanaume UPUPU hata kaa na wewe, hata akikuoa lazima chepuka kwakua hajisikii kama mwanaume mbele yako. Najua huamini ila kama unamhonga mwanaume chunguza kidogo tu lazima anchepuka na kuna sehemu anahonga tena sana tu.
Halafu unafikiri hata una haja ya kutumia nguvu kubwa, hapana rafiki zako wote wanajua kuwa anachepuka na wanakuchora tu. Ni ngumu sana mwanaume kutulia analishwa na kuvishwa na mwanamke, anahudumiwa kila kitu na mwanamke, hajisikii raha hajioni mwanaume! Ni matumizi mabaya kabisa ya uanaume wake!
👌
0 Maoni