My dia Nisikilize

Related image


Katika kuongea na wanawake wengi ambao huniomba ushauri nimegundua kitu kimoja, chanzo kikubwa cha mateso ya wanawake si ukatili wa wanaume bali ni kushindwa kuwa huru kikipato.

Kuna wanawake wengi ambao huvumilia mateso kwakua tu hawana namna ya kufanya, kwamba wanaume wao wamekua ni kama mabosi wao, mtu huwezi kuacha kazi kwakua hujui kama utakula wapi?

Hapa sizungumzii tu wale ambao hawana ajira, hapana hata wale ambao wameajiriwa wengi unakuta wamekua wategemezi kwa wanaume. Hii hutokea kwasababu mbili, kwanza nikwakua wanamatumizi makubwa kuliko vipato vyao.

Kwamaana kua kama mwanamke hufanya kazi ambayo humuingizia mshahara wa shilingi laki tatu unakuta matumizi yake ni ya laki sita. Hii ikimaanisha kua atamtegemea mumewe kwa shilingi laki tatu ya ziada.

Kwa maana hiyo basi anaona kama akiondoka basi kuna vitu vingi vya laki tatu mbavyo atavikosa. Hili ni tatizo kwani anakua ameshavizoea vile vitu mpaka anashindwa kuviacha, kwamba mwanamke aliyezoea Gari kumuambia atembee kwa miguu anaona bora kuteseka.

Utegemezi mwingine kwa wale wanaofanya kazi hutokea pale ambapo mwanamke anaingiza kipato sawa lakini chote kinatumika katika kulea na kuchangiaa mendeleo ya familia. Mwisho wa mwezi anajiikuta hana akiba yoyote hivyo kuona ugumu kuondoka.

Lakini pia amechangia sana katika familia, kwa mfano amechangia katika ujenzi, amechangia katika biashara na maendeleo mengine. Anaona kua akiondoka basi atapoteza kila kitu.

Lakini kwani tufike kote huko, kwanini tuwaze kuondoka na sikuwa na furaha katika ndoa, mwanamkie ukiwa huru kikipato (sio kufanya kazi, kuwa huru kikipato) basi ni ndoto kwa mwanaume kukunyanyasa.

Mwanamke ni lazima uanze kufikiria namna ya kuwa huru kikipato. Hapa nikimaanisha sio ufanye kazi tu, lakini uwe na uwezo wa kujitegemea hata kama mwanaume hatatoa chochote, kwamba pesa zako zisiishie katika kununua nguo, kwenda saluni na vitu vyakupita. Hapana lakini uanze kuwaza namna ya kuwekeza katika vitu vya msingi, biashara, nyumba na hata katika elimu ya wanao.
... Amuka nielewe..

Chapisha Maoni

0 Maoni