Mhimu Kwa wale wenye mapenzi ya mbali SOGEENI HAPA

Related image

Kama mna mapenzi ya mbali na manataka msiboane hembu tafuteni umbea wa kuzungumzia mara kwa mara, ndiyo nimesema umbea. Wakati mwingine mkizungumzia mambo yenu inachosha, mambo ya kuulizana umevaa nini sijui umekula nini kila siku inaboa, tafuteni kitu ambacho kitawalazimisha kuzungumza hata nusu saa masaa mawili, kwamba hata kama mtu yuko bize namna gani lakini stori zinoge.

Kwa mfano kuna yule jirani yenu, mzungumzieni, msengenyeni hamna namna nani alimuambia awe anagombana na mke wake kila siku! Kuna yule bosi wenu mwenye kiherehere, mzungumzieni msengenyeni weee ndiyo maisha (kama ni dhami mimi sipo). Lakini pia tafuteni kitu cha pamoja, labda mpira, mkazungumzia usajili wa Yanga na namna wanavyohaha na vilima vyao Jangwani pale, mkazungumzia mipango ya Simba kuingia nusu fainali na hata fainali kilabu bingwa.

Siasa, hata umbea na udaki, tafuteni kitu cha kuchangamsha mazungumzo yenu cha pamoja. Mara nyingi hivi vitu vinakuja tu lakini kama havipi vitafuteni. Kuna watu wanataka kuongea kila saa lakini hawana chakuongea, wakipigiana simu ni “Niambie... sasa … kwahiyo… umesha kula… umeme umeisha…” unaweza kulalamika kuwa mwenza wako haongei na wewe lakini ukichunguza unakuta hata hana kitu cha kutakiwa kuongea na wewe!
JIFUNZE UBUNIFU
MFANYE AWE MU MBEYA WAKO
Siyo kila siku, wewe ni lawama tu
Mbona unachelewa kujibu sms
Ina maana hujaona simu yangu
Ndio unanijibu saivi muda wote huo
Na kununa nuna tu ovyo
HAPO UTAFELI

Chapisha Maoni

0 Maoni