JE WEWE NI MCHEPUKO, UNAJUA WANAUME WANAPELEKA WAPI PICHA/VIDEO ZA UCHI ZA MICHEPUKO YAO?

Image may contain: 1 person, smiling, standing and shoes


Moja ya sifa kubwa ya mwanaume rijali ni kuwa na wivu kwa mwanamke ambaye anampenda, hii ndiyo maana wanaume wengi wanafurahia kuona picha za uchi za wanawake lakini si picha za uchi za wanawake wanaowaheshimu. Lakini pia hawatapenda kuona picha za uchi za watu wanaowaheshimu zikionwa na watu wengine, huwezi kuona mwanaume anaonyesha washikaji zake picha za uchi za mkewe, dada yake, Mama yake au ndugu yake anayemheshimu.
Tukiachana na ndugu ni ngumu sana kuona mwanaume eti anamuongelea mke wake mbele ya marafiki zake, anasifia maumbile yeke na hata kuonyesha picha za uchi au za kudhalilisha. Lakini labda niwaambie tu dada zangu, kila siku wanaume huonyeshana mapicha ya uchi ya wanawake anaotembea nao. Sasa unajiuliza hao wanawake ni wakina nani na kwanini wanaonyesha, basi hao ni michepuko ambao wanaume huwaona kama Malaya.
Sasa kama wewe ni mwanaume, unatembea na mume wa mtu au mwanaume ambaye unajua kabisa anamchumba wake na alishakuambia anamchumba na kweli unamjua na unajua wanapendana, halafu huyo mwanaume akakuomba picha zako za uchi au mko chumbani akachukua video anafanya nawewe mapenzi. Tena hili ndiyo kubwa zaidi kwamba kama anachukua video anafanya na wewe mapenzi au anakuchukua unacheze mwili wako basi jua anakwenda kuonyesha kwa marafiki zake.
Kwanza kabisa unatakiwa kujua kuwa amekudharau kwanu anajua simu yake wanashika washikaji hivyo hata kama asipowaonyesha basi wataziona. Kwa maana hiyo hajali kabisa kama uchi wako ukionekana dhahiri kwa watu, lakini pili inawezekana anachukua makusudi ili kupeleka kuonyesha kuwa anatembea na wewe, kuonyesha jinsi ulivyokicheche na kama kweli anafanya hivyo basi jua hawezi kukuoa, huwezi kumpindua mkewe na hawezi kuwa na mwanamke kama wewe.
Ni ngumu sana kwa mwanaume kuwa na mwanamke ambaye anajua rafiki zake wote washaona maungo yake. Hivyo kama wewe ni mchepuko unapotuma picha ya uchi au ukachukuliwa video basi jua unaenda kudhalilishwa sehemu. Fanya hivyo ukijua kuwa huyo mwanaume hawezi kuwa na wewe kwakua rafiki zake wanajua kila kitu katika mwili wako. Yes kwa mwanamke wa kupita hatajali sana ukidhalilika lakini si mkewe au mwanamke anayempenda hivyo unapokubali huo ujinga basi jua unatumika tu kwa muda!

Chapisha Maoni

0 Maoni