
Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia
siha njema na pia kwa kunipa mwangaza wa
kuandika hiki ninachokusudia. Pia niwashukuru
wapenzi wasomaji wa safu hii ambao tumekuwa
tukiwasiliana na kushauriana hili na lile katika
tasnia hii adhimu ya mapenzi. Nawakaribisha
sana!
Labda kwa wale wasiofahamu niwaambie tu
kwamba dhana ya mapenzi ni dhana yenye wigo
mpana sana na ndiyo maana hutasikia hata siku
moja tumepumzika kuizungumzia.
Hata hivyo, tunachofanya siku zote ni
kukumbushana kwa yale tunayoyafahamu na
kushauriana kwa pale tunapohisi wengi hufanya
makosa.
Baada ya kusema hayo sasa nigeukie mada
yangu ya leo ambayo kwa kiasi kikubwa
inawahusu wale walio kwenye ndoa na kikubwa
nazungumzia yale ambayo wawili waliotokea
kupendana kwa dhati wanatakiwa kuyafanya
mara baada ya kumaliza kufanya tendo la ndoa.
Nalazimika kuandika makala haya baada ya
kubaini kuwa wengi wamekuwa wakifanya
makosa na kujikuta wakishamaliza kufanya tendo
hilo takatifu, kila mmoja anageukie kwake kisha
kuuchapa usingizi.
Sisemi kwamba ni lazima kuyafanya haya
nitakayoyaeleza leo ila yakifanywa huwa na
manufaa yake na mara nyingi yanaboresha
uhusiano.
Kuoga pamoja
Mtakuwa ni watu wa ajabu kama mtamaliza
kufanya tendo hilo kisha kila mmoja kulala na
majasho yake. Wapo wasiojali katika hili na
kuona kuoga au kutooga ni uamuzi wa mtu.
Elewa linapokuja suala la usafi inashauriwa
mkimaliza lazima muoge.
Wapo wanawake ambao wakishamaliza
hukimbilia kuwaandalia maji wenza wao,
wakishaoga ndipo nawo huenda kuoga. Hivi
unaona ugumu gani kwenda kuoga na mwenza
wako? Unaijua raha ya kuoga na huyo wako wa
maisha?
Wanaofanya hivyo wanajua raha yake na wewe
ambaye hujawahi, anza leo. Mmemaliza mambo
yenu, chukuaneni kimahaba, elekeeni bafuni kisha
ogeshaneni kimahaba.
Baada ya hapo rudini chumbani, mkishajifuta maji
pandeni kitandani mkiwa wapesi.
Kusifiana
Hakuna muda maalum uliotengwa kwa ajili ya
wanandoa kusifiana. Hilo linaweza kufanyika
wakati wowote lakini pale mnapomaliza kufanya
0 Maoni