
Kuna aina nyingi za kuelezea Usaliti/Uongo katika mahusiano,lakini zadi ni kitendo na hiali kinachofanywa na mtu mwenye lengo na nia ya kupata au kujifaidisha au kukwepa jambo Fulani kwa manufaa yake binafsi, ni kitendo cha kuvunja hali ya uaminifu na kutokuwepo usawa.
Kwa % kubwa watu wanao saliti wenza wao hufanya wakijua kwa akili timamu kabisa na hujipanga na kutengeneza mbinu zaidi, msaliti anaweza kutumia masaa, siku ,week, mwezi hata na zaidi kupanga mission ya kufanya usaliti, hivyo sio jambo la bahati mbaya. (Omarzu, J. 2000)
Nje na msukumo wa mihemko ya hisia za mapenzi,watu wengi wanao shuhudia usaliti wanasema kwamba kuna sababu mbalimbali zinazosababishwa na wenza wao wa mwanzo, hivyo kufanya MAHUSIANO yaonekane sio salama na kuamua kutafuta huduma hiyo sehemu nyingine.
Katika kuzungumza na watu mbalimbali wakiwemo watu wanao jihusisha na kusaliti wapenzi wao, wengi wao wametaja sababu zifuatazo kama msukumo wa usaliti katka MAHUSIANO mengi.
1. Kutoridhika kimahaba katika mahusiano ya mwanzo, ikiwa mwanamke au mwanaume hashibi na kukata kiu yake ya tunda basi hupelekea njaa nyingi na yenye msukumo mkubwa dhidi ya mhusika na kusababisha usaliti ili aweze kukidhi njaa (sexual dissatisfaction in a primary relationship).
2. Tendo la ndoa kuwa kama starehe, wengine hufanya mazoea ya tendo la ngono kama starehe, hali hii hupelekea uhitaji wa mara kwa mara na kuwa addicted zaidi na kila mtu anae muona wa jinsia tofauti na yake kama anaweza kumtimizia haja yake, hivyo hupekea hali hiyo.
3. Kukosa hisia na kujiona kama umetengwa na MWENZI ,hii hutokana na tabia mbalimbali ambazo pengine sio nzuri zinazofanywa na baadhi ya wapenzi nakupelekea hali ya kuamusha hisia hasi kwa mpenz hivyo kupelekea MTU kutafuta mwingine kwa ajiri ya kuziba gap la MAUMIVU.(lacking a romantic connection to your primary partner)
4. Kupenda mwonekano kwa mtu mwingine, wasaliti wengine hupatwa na msukumo wa kusaliti iwapo wanakuwa wamekinai na kuchoka mwonekano wa wapenzi wao walionao( usiobadilika) mara nyingi wengi wanasema zadi katika mambo ya uchafu, kujipamba na maumbile. Hivyo mwonekano mpya huvuta hisia za kutaka kuona utofauti uliopo katika mahusiano mengine.
5. Kufanya kisasi kwa mwenza aliewahi kukusaliti, katika vijana wengi hutenda usaliti pia kwa kufanya revenge kwa wapenzi wao kwa maana ya kuwakomoa ama kushindana nao, kiwango cha maisha ya kujitegemea kiakili hupungua na kujikuta wanaishi katika maisha ya watu na hisia za wa watu wengine na kuendeshwa kama gari.
6. Kutafuta uzoefu (experience) mpya katika mahusiano mengine, walio wengi katika hili huwa hawana uhakika na MAHUSIANO yao kama ndiyo MWISHO wa uhitaji wa kimapenzi,hivyo hutaka kuangalia sehemu nyingine ekwa ajiri ya Ku experience nini jipya katika mahusiano yao, na mara kadhaa hukutana na vitu vipya zaid vianvyowafanya wakomae na kuwa wakomavu KATIKA kusaliti wenza wao.
Haya mahusiano ya ziada (Extramarital relationship affairs) au usaliti na udanganyifu katika mahusiano yanonyesha kuwa kuna mambo magumu zaidi ya hizo SABABU NA MAANA ZAKE hapo juu ambazo haziwezi kutokea pasipo kuwepo ugomvi wa ndani kwa ndani (intrapersonal conflicts) au ugomvi wa mtu na mwenzie (interpersonal conflicts), na usaliti ukishaingia ndani ya mahusiano ni rahisi kutenganisha hisia na mvuto kati ya wawili.
Msaada
Sio kila MTU anaesaliti na anaesalitiwa ana mapungufu binafsi yasiyoweza kusababishwa na mwenza wake bali huenda ni sababu ya kutoka pande zote mbili au upande mmoja tu, kumbe maamuzi ya kusaliti yanaweza kusababishwa na msaliti au msalitiwa kulingana na jinsi wanavyoendesha mahusiano yao!. Na ukigundua una salitiwa basi ni vema kabla ya maamuzi yeyote ukae na kujitathimini kwanza wewe kabla ya kutoa hukumu na kusukuma lawama zote kwa mwenza wako.
0 Maoni