
Aliyesema Ndoa ndoano hiv huyu mjinga ni nani ?? Poleni Mapasta mnaosimamia Ndoa , polen kwa ujinga mnaosimamia ,mngesimamia ukucha mngekuza hata familia , kam ni pete nisharudisha Kwa sonara , nimeshavuta mpunga ,nimesharudisha busy ya hasara , Kabla ya kuingia ndoani anakuwa kondoo usiemjua , ukishamuingiza ndani anakuachia mabua .. Umeshawahi kuingia kwenye mahusiano ambayo hujui yanahusiana nanini ?? 😀😀 Haya ni baadhi ya mistari kwenye ngoma mpya ya Stamina ft Atan "Asiwaze .
.
Mc pilipili yupo right kabisa kwanini umetuhusisha kwenye kuvunjika kwa ndoa yako? Km ndoa imewashinda unamuambia nani? Kwa faida gani? Na ili iweje kwa mfano?
Mbona wakati unamtongoza, ukamchumbia, ukamvisha na pete hatimae kumuoa hukutuambia zaidi ya kuona hizi 👇picha mitandaoni? Leo kitu kimebuma fasta umekimbilia studio kulialia dunia nzima ijue ili uonewe huruma au? Kama wewe ndio ulikuwa chanzo cha yote kutokea si tutajuaje? Au sababu yule dada hana pa kusemea? na wewe ukatumia mwamvuli wako wa usanii kuanika ubaya wa mwenzio wa kwako nani atatuambia? Au unataka kutuaminisha kwenye hiyo ndoa wewe ulikuwa ni malaika?
Kwani ni ndoa ngapi zimevunjika nchi hii za watu mashuhuri na za watu wa kawaida kwenye jamii yakwako ndio ya kwanza? Nyinyi celebrities ndivyo mlivyo mnaoa na kuolewa kwa siri ila mkiachana dunia nzima mnataka ijue why?
Ifike kipindi mjitambue sio kukurupuka kutafuta attention za watu kisa mnajulikana. Natamani huyu dada popote alipo aje aite hata press conference tumsikie na yy ana lipi la kusema naamini anayo km mwenzake kamwaga mboga yy akipindua ugali kuna shida?
Hii imekuwa ni desturi sasa kwa wasanii hasa wa muziki wanapoachana na wenza wao hukimbilia studio kutafuta huruma za wananchi. Juma nature alipoachana na aliyekuwa mchumba wake Sinta akaja na wimbo Sitaki demu, Lady jay dee alipoachana na mumewe Gadner akaja na wimbo Ndi ndi ndi, na wengine nimewasahau leo Stamina kaja na Usiwaze hebu badilikeni mnavyojua kuyaanza kimyakimya muyamalize hivyo hivyo watu tuna stress NIDA inatuchanganya hatujui hiyo tarehe 20 itakuwaje bado hatuna no na laini zetu tunazipenda
0 Maoni