Mapenzi ya Sultan Süleyman na Hürrem Sultan

Mapenzi ni kama moto unaowaunguza wapendanao.Ni maafa yanayoweza kuangamiza...


Mapenzi ya Sultan Süleyman na Hürrem Sultan

Mapenzi ya Sultan Süleyman na Hürrem Sultan yalikuwa ya kweli na ya dhati. Hürrem aliyebadilisha maisha ya mfalme alikuwa ni binti wa Kirusi mwenye umri wa miaka 17. Mfalme wa Ottoman alizaliwa watoto na mkewe kabla ya kupoteza maisha.
Baadaye Suleyman Han akakutana na Gülfem ambaye ni kijakazi wa kasri aliyemuondoa upweke na kumliwaza kutokana na majonzi yaliyokuwa yakimuandama hadi kufikia umri wake mkubwa.
Süleyman alimpenda Gülfem kupindukia kiasi cha kutaka kuwa naye pekee kuliko mwanamke mwengine yeyote.
Ndoto kubwa walioyokuwa nayo Vijakazi wote wa kike katika kasri ilikuwa ni kupendwa na mfalme.
Na wale waliobahatika kupendwa na wafalme basi huishilia kuwa na utajiri. Wote walikuwa na hamu ya kuwa karibu na Sultan Süleyman kama alivyokuwa Hürrem Sulatn lakini Gülfem ndiye aliyeonekana kuwa na bahati ya kuchukua nafasi ya Hürrem Sultan. Gülfem alianza kuonewa wivu na vijakazi wenzake.
Kama alivyokuwa akimfanyia Hürrem, Süleyman Han pia alikuwa akimwekea Gülfem hifadhi ya akiba ya raslimali 6 hadi 150.
Gülfem akaanza kukusanya fedha na raslimali hiyo kila siku ili kutimiza ndoto yake kubwa ya kujenga msikiti, maktaba na madrasa. Hata kama hangeweza kufanikisha vyote, basi alitaka angalau aweze kujenga msikiti kwa ajili ya Allah.
Hatimaye alipokusanya fedha za kutosha, akaweka msingi wa msikiti mmoja Üsküdar. Gülfem alikuwa ni mwanamke aliyemheshimu Sultan Süleyman kama mfalme licha ya kuwa mumewe.
Alikuwa msiri aliyewaelezea watu wachache pekee kuhusu mpango wake wa kutimiza ndoto zake za kufanya kazi za kheri kama kujenga msikiti.
Sultan Süleyman hakuwa na habari kuhusu ujenzi wa msikiti wa Üsküdar.
Muda mchache baada ya kujenga msikiti bila mtu yoyote kujua, pea zikamwishia Gülfem. Hazikutosheleza kukamilisha ujenzi wa msikiti huo.
Gülfem hakuwa na akiba yoyote na hakujua cha kufanya. Baada ya kujikuta katika hali ile, akataka kumwelezea Sultan Süleyman mradi wake wa msikiti alioshindwa kuumalizia. Lakini alishindwa kusema kwa kudhania kwamba lingekuwa jambo la aibu kwake.
Hakutaka kuomba pesa mtu yeyote kutokana na kuepuka aibu kwa kuwa alikuwa mtu mwenye hadhi ya juu.
Hali ilipozidi kuwa ngumu, Gülfem akaamua kuomba msaada kutoka kwa vijakazi wa kasri.
Akapokea wazo la kustaajabisha kutoka kwa kijakazi mmoja.
Mfanyakazi huyo alitoa ahadi ya kumsaidia Gülfem kwa kiasi kikubwa iwapo angemkubalia kuchukuwa nafasi yake na kuwa na mahusiano na mfalme Sultan Süleyman. Kutokana na hamu yake kubwa aliyokuwa nayo Gülfem ya kutaka kukamilisha ujenzi wa msikiti aliouanza kuujenga, akakubali pendekezo hilo.
Je, angewezaje kuhakikisha utekelezaji wa jambo hilo pasi na mfalme kujua? Gülfem aliwaza na kuwazua sana suala hilo lililomtia huzuni moyoni. Alilazimika kutafuta suluhisho kuhusu suala hilo lenye utata.
Usiku mmoja, wakati mfalme alipokuwa chumbani akimsubiria Gülfem, alishtuka kumuona kijakazi badala yake. Mfalme akamuulizia Gülfem. Kijakazi huyo akamwambia mfalme kwamba Gülfem alikuwa kwenye matibabu na usiku huo ukapita hivyo.
Hata hivyo, Gülfem alitambua kuwa baada ya siku kadhaa mambo huenda yakafichuka na kumletea tabu. Lakini Sultan Süleyman akaanza kufikiria kwamba Gülfem alikuwa akijaribu kujitenga na kukaa mbali na yeye. Kila mara Gülfem alikuwa akitoa sababu tofauti kwa mfalme.
Gülfem alishindwa kujieleza mwenyewe kwa mfalme kutokana na kuogopa kusema uongo. Hivyo basi akawa anamtumia kijakazi yule aliyeleta wazo hilo kumtetea yeye kwa ajili ya kutimiza mahitaji yake.
Usiku mmoja wakati mfalme alipokuwa akimsubiria Gülfem, akaja tena yule yule kijakazi.
Sultan Süleyman akahamaki kukasirika mno huku akisema kwamba amechoshwa na sababu alizokuwa akipewa kuhusiana na Gülfem kushindwa kuwa naye kama ilivyokuwa tangu zamani. Alikuwa ni mzee ambaye hakutaka kuhangaika na vijakazi wa kasri.
Sultan Süleyman alipotaka kujua ukweli wa mambo, hakuambiwa kwamba Gülfem alikuwa akifanya hivyo kwa ajili ya fedha ili aweze kukamilisha msikiti aliokuwa ameanza kuujenga.
Hivyo basi, mfalme akajuwa kwamba Gülfem alikuwa akimdanganya kimapenzi na kumtia hasira mno. Hakuamini iwapo mwanamke aliyempenda kwa dhati na kumthamini angeweza kumfanyia kitendo kama hicho. Baadaye mfalme akamuamuru mkuu wa kasri kumchukua Gülfem na kumuadhibu kwa kumdhalilisha mfalme.
Mkuu huyo wa kasri ambaye hakujua kilichokuwa kikiendelea akafuata amri ya mfalme na kumchukua Gülfem. Alikamatwa na kulazwa kifudifudi kisha akaanza kucharazwa mijeledi kwa nguvu kama alivyoamrisha mfalme Sultan Süleyman. Gülfem alishindwa kueleza ukweli licha ya kuzongwa na maumivu kutokana na adhabu kali.
Hatimaye maumivu yakazidi na akakata roho ghafla.
Baada ya Sultan Süleyman kupokewa taarifa za kifo cha Gülfem, akahuzunika mno. Jambo lililomfanya kuumia zaidi ni baada ya kugundua ukweli wa mambo. Alijilaumu kwa kumuadhibu Gülfem kwa sababu ya dhana mbaya aliyokuwa nayo dhidi yake kinyume na nia yake njema ya kutafuta msaada wa fedha ili kukamilisha msikiti. Hakuwa na la kufanya wala hakuweza kumrudisha tena Gülfem.
Kilichobaki ni mfalme kukamilisha ujenzi wa msikiti ulioachwa na Gülfem. Sultan Süleyman akampa maagizo Mimar Sinan akamilishe msikiti ule na kujenga maktaba na madrasa pembeni mwake.
Bi Gülfem naye akazikwa katika kaburi lililojengwa ndani ya msikiti huo. Juu ya kaburi hilo kukaandikwa maandishi haya “shujaa.”

Chapisha Maoni

0 Maoni