INAENDELEA HAPA:Kipindi Mr. Brown anampiga mke wake Mrs. Brown ghafla wakatokea wazazi wa Mr. Brown ambao ni wakwe wa Mrs. Brown walikwenda kuwatembelea wakakuta kuna vurugu kwa watoto wao walichokifanya wazazi wale waliamua ugomvi na kuwaweka chini na kuwasikiliza kwa umakini watoto wao chanzo cha wao kugombana ni nini? Wakaanza kuelezea ilivyokua. Wazazi wa Mr. Brown wakatumia busara na kuwasihi wasigombane na wakawapatanisha watoto wao pale pale Mr na Mrs. Brown wakamaliza tofauti zao wakawa na amani wakajumuika pamoja na wazazi wao mpaka ilipofika jioni wale wazazi wakaondoka huku nyuma Mr na Mrs. Brown walikaa na kujadili njia nyingine ya kumsaidia binti yao Jenifer aweze kuendelea na masomo shule wakaona ni bora wamtafutie tu binti yao shule nyingine ili aweze kuendelea na masomo yake, baada ya siku kadhaa Mr. Brown alijitahidi kuhangaikia shule ili aweze kumpeleka binti yake JENIFER aweze kuendelea na masomo akiwa na dhamira ile ile aliyokua nayo tangu awali kuwa binti yao JENIFER wakimsomesha baadae atakuja kuwasaidia katika maisha yao, mungu alisaidia Mr. Brown akajitahidi akafanikiwa kumpatia nafasi binti yake JENIFER katika shule moja iitwayo KILIMANJARO SECONDARY SCHOOL na binti yao akajiunga na shule hiyo akaendelea na masomo yake. JENIFER alipokua shuleni hapo tabia yake chafu haikubadilika aliendelea na tabia yake ile ile ya kua na marafiki ambao tabia zao zilikua ni chafu na ikafikia hatua JENIFER akawa anamahusiano ya kimapenzi na waalimu wa shuleni hapo tena kwa kuwachanganya alikua anatembea na MWALIMU MKUU (head master), MWALIMU MKUU MSAIDIZI (Second master) na MWALIMU WA TAALUMA (Academic master) tena bila ya walimu hao kutofahamu kama wanachangia penzi moja kwa binti huyo, Sasa siku moja Mwalimu mkuu wa Shule hiyo ambae ni mpenzi wake JENIFER alimuita JENIFER ofisini kwake na kuanza kumshika shika ofisini hatimae wakafanya nae tendo chafu la ngono ndani ya ofisi na hawakufunga mlango wa ofisi hiyo, ghafla Mwalimu mkuu msaidizi akafungua ule mlango wa ofisi ya mwalimu mkuu, alikua anampelekea ma faili mwalimu mkuu alipovamia akamkuta mwalimu mkuu na JENIFER wakiwa katika tendo, mwalimu mkuu msaidizi alishtuka sana kuona vile hakuongea kitu alitoka nje haraka.
JAMANI MIE UKAHABA SASA BASI"PART 5
INAENDELEA HAPA: Baada ya kuvutana sana kati ya Mwalimu mkuu na Mr. Brown ofisini ikabidi mwalimu mkuu akubali kuwa mpole na kurudisha pesa japo sio zote ilibidi mwalimu mkuu atoe nusu ya pesa zilizolipwa, Mr. Brown alilipa ada Shilingi laki moja na nusu ikabidi mwalimu mkuu atoe nusu ya pesa hizi Shilingi elfu sabini na tano na kumpa Mr. Brown. Mr. Brown akapokea zile pesa Shilingi elfu Sabini na tano akamchukua binti yake JENIFER wakaondoka na kuelekea nyumbani kipindi wapo njiani wanaelekea nyumbani, Mr. Brown alikua na hasira sana akamwambia binti yake JENIFER "We mtoto leo tukifika tu nyumbani chukua nguo zako na uondoke nyumbani kwangu sitaki kukuona, mshenzi wewe!". Walipofika nyumbani tu Mr. Brown akaanza kumuhadithia mke wake Mrs. Brown yaliyotokea shuleni kuhusu binti yao JENIFER na akamwambia Mrs. Brown kuwa hataki hata kumuona aondoke nyumbani kwake lakini kwa maamuzi haya ya Mr. Brown mke wake Mrs. Brown hakuafikiana nayo akamwambia mume wake "SASA MUME WANGU UNAMFUKUZA MTOTO AENDE WAPI WAKATI HAPA NDIO KWAO, UNADHANI ATAENDA WAPI? KAMA MAJI YAMEISHAMWAGIKA MAKOSA NDIO KISHAFANYA HAKUNA JINSI NI KUMSAMEHE NA TUKAE TUSHAURIANE TUJUE TUNAFANYAJE MUME WANGU PUNGUZA HASIRA". Mr. Brown akamjibu "HAIWEZEKANI MIMI SITAKI HATA KUMUONA HUMU NDANI AONDOKE SITAKI KUMUONA". Mrs. Brown nae akamjibu "KAMA UNATAKA HUYU BINTI AONDOKE HUMU NDANI BASI JUA NITAONDOKA NAE SIWEZI KUKUBALI BINTI YANGU AONDOKE AKAPATE SHIDA WAKATI KWAO ANAPO, UKIMFUKUZA JUA NAMIMI NAONDOKA HUMU NDANI" Baada ya Mrs. Brown kumuambia Mume wake Mr. Brown maneno hayo ghafla Mr. Brown alisema kwa sauti kali ya juu "SAWA MKITAKA MUONDOKE WOTE, SIWEZI KUFUGA UPUMBAVU KAMA UNAONA NAMUONEA MTOTO WAKO MFUATE MUONDOKE WOTE PUMBAVU!". Mrs Brown akamjibu "EH E! TAFADHALI BABA WEE, USINITUKANE NGOJA TUKUPISHE UBAKIE NA NYUMBA YAKO SIO UNIFOKEE. MPUMBAVU MWENYEWE!. Ghafla Mr. Brown alikurupuka na kumvamia mke wake Mrs. Brown na kuanza kumpiga makofi huku akimwambia "YANI WEWE UNADIRIKI KUNIAMBIA MIMI MPUMBAVU, WAKATI JENIFER KAFANYA MAKOSA DHAHIRI. HIVI MIMI NINAVYOHANGAIKA KUTAFUTA PESA ZA KUMSOMESHA HALAFU ANALETA UPUMBAVU UNAFURAHIA ETI EEH!"
UMEWAHI kujiuliza; kwanini mastaa wengi hawadumu na wenzi wao? Nimeamua kuchambua mada hii kwa sababu tunao mastaa wengi kwenye jamii yetu ambao wana uhusiano ama na mastaa wenzao au watu wa kawaida.
Pia, wapo watu ambao wanatarajia kuwa na uhusiano na mastaa, wakati kuna ambao tayari wapo ndani ya penzi na watu maarufu. Pamoja na hayo yote, wengi huwa wanashindwa kudumu kwa muda mrefu na mastaa kwa sababu za hapa na pale. Katika mada hii ambayo nimeifanyia utafiti wa muda mrefu, itakufanya mpya katika uamuzi wako, ndani ya uhusiano na staa au staa ambaye yupo katika uhusiano na mwenzi asiye staa. Labda tuwekane sawa kidogo, hapa namzungumzia mtu maarufu katika jamii, maarufu kwa maana ya kujulikana sana. Ustaa wa mtu unaweza kusababishwa na kazi au sanaa. Mathalani, sanaa za maigizo, soka, ndondi, riadha, siasa, urembo, utangazaji, uandishi wa habari, mitindo, utunzi, uchoraji, uchongaji, biashara nk. Siwezi kutaja moja kwa moja majina ya mastaa, lakini naamini nimeeleweka vyema kuwa nawazungumzia watu wa aina gani. Watu wanaojulikana sana katika jamii kulingana na kazi zao za kila siku. WASIKIE MASTAA Wakati naandaa mada hii, nilipata bahati ya kuzungumza na baadhi ya mastaa ambapo walitoa maoni yao. Kwa bahati mbaya sana, wote niliopata kuzungumza nao, walipojua mazungumzo yetu yangeishia kuwa mada gazetini waliomba kuhifadhiwa majina yao. Hebu wasikilize: “Kiukweli kaka Shaluwa, naweza kusema sisi wanawake wenyewe ndiyo wenye matatizo...asikudanganye mtu, ustaa kazi. Ukishakuwa maarufu, unataka mambo mengi; vipodozi, gari, nguo mpya, kujirusha, simu iwe na full vocha nk. “Sasa kama unakuwa na boy ambaye anajifanya anakuchunga sana, inakuwa ngumu kudumu na sisi tulivyo jeuri, akikuacha asubuhi, jioni kiwanja unakutana na mwingine.” Huyu ni staa wa muziki wa dansi nchini kama alivyozungumza nami jijini Dar es Salaam hivi karibuni. “Kiukweli huwa tunaacha sana mademu, lakini siyo suala la umalaya hapo brother Shaluwa. Kuna mambo mawili makubwa; kwanza, mwanamke anakuwa anapenda ustaa wako na siyo penzi la dhati, pili anakubana na kukupangia sana ratiba...niseme kwamba, wivu unazidi! “Unajua unapokuwa msanii, unakuwa na mambo mengi, shoo kibao kila week-end, safari za mikoani nazo hazina idadi, club ndio usiseme, sasa kwa hali hiyo, lazima uwe na mwanamke smart kwa kila kitu. “Tuongee ukweli, hakuna mtu anayekubali kuwa na mpenzi tapeli, sisi hatuna matatizo, lakini kama umefuata jina langu au pesa, nitakushtukia soon na hapo ndipo nitakapompiga kibuti na maisha yanaendelea,” ndivyo mmoja wa kinara katika Bongo Fleva anavyosema. Hebu sikia kauli ya msanii huyu wa filamu: “Wanawake wanapenda umaarufu wetu, kwahiyo ukiwa naye siku mbili, ukimshtukia unamtema, hapo ndipo penye tatizo bro. Mimi sihitaji mtu anayependa jina langu, nahitaji penzi la dhati.” TATIZO NI NINI? Kikubwa ni katika KUELEWA na kutofautisha mapenzi na ustaa. Kama umempenda, umpende kwa mapenzi ya dhati, achana na ustaa wake, lakini lazima umjue mwenzi wako na uende naye jinsi anavyotaka. Mapenzi ya kitapeli au kufuata mali na umaarufu hayana nafasi kabisa katika maisha ya sasa, yote yanawezekana lakini kwa kukubali kujifunza na kubadilika kulingana na mwenzi wako alivyo. UPO KWENYE UHUSIANO NA STAA? Kama nilivyotangulia kusema awali, sina maana kwamba mastaa wote hawawezi kuishi na wenzi wao bila kuwepo kwa migogoro, ni baadhi yao! Pamoja na kuwa na migogoro hiyo ambayo mwisho wake mara nyingi imekuwa ni kuachana, hakumaanishi kwamba, mastaa hawafai kuwa na wapenzi. Hapa nataka kuzungumza na wale ambao tayari wapo katika uhusiano na mastaa na wale ambao wanatarajia kuwa na wenzi wenye majina makubwa kwenye jamii. Hebu pitia vipengele vifuatavyo; Usiwe na wivu sana! Ni kweli kwamba, kati ya alama za mapenzi ya dhati ni pamoja na wivu, lakini unapokuwa na uhusiano na mwenzi staa, lazima upunguze wivu. Hii haina maana kwamba, umuache awe kicheche, awe na mapatna wengi, hapana! Mara nyingi mastaa huwa wanaiga mambo ya Kizungu, mathalani husalimiana kwa kukumbatiana, kuandikiana sms kwa maneno ya mapenzi kama dear, sweetie, mpenzi n.k, ukikutana na mazingira kama hayo, kuwa mpole, lakini fanya uchunguzi wako taratibu bila ya yeye kujua. Penye ukweli, uongo hujitenga.
0 Maoni