
Nisikilize
ANGEKUA ANAKUPENDA SANA ANGEKUOA WEWE ACHA KUJIDHALILISHA KWA KUKUBALI KUTUMIKA!
Baadhi ya wanaume wanadhani kua wanahaki ya kuwaacha wanawake na bado kuendelea kuwatumia kimpenzi au katika mambo yao na kwa bahati mbaya zaidi kuna wanawake wengi huona kama ni raha, huona kama ni kumkomoa mtu mpya, mke au mpenzi kwa kuendelea kutumika kimapenzi baada ya kuachika, baada ya kuumizwa.
Mwanaume kakuacha kaoa mwanamke mwingine na ana maisha yake lakini bado bila aibu anakuja na kukuambia nimekukumbuka, nimeshindwa kukusahau sina furaha na huyu wa sasa. Anakutumia kimapenzi lakini wakati huo huo bado yuko na mtu wake awe mpenzi au mke. Halafu usivyo na akili unajidanganya kuwa “Amekuoa wewe lakini bado ananipenda mimi!” Dada yangu wewe unalaana tu.
Mwanaume anayekupenda hawezi kukufanyia hivyo, hawezi kukuacha kwa sababu yoyote ile na kama akikurudia na kweli akakupata si kwasababu anakupenda sana, sikwasababu wewe ni mtamu kuliko ma X wake wote hapana nikwakua kati ya ma X wake wote wewe ndiyo ‘Maharage ya Mbeya’ ambaye hujui thamani yako, ambaye anaweza kukutumia kiongono huku akirudi kwa mkewe au mpenzi wake.
Iko hivi wanaume wengi wanapenda vitu rahisi, kwamba gharama za kutongoza mwanamke mpya ni kubwa kwani zinahitaji mchakato wa muda na kuhonga pia. Kwa maana hiyo kuliko kutafuta mchepuko mpya ni bora kufufua makaburi kwani mpenzi wa kale hana gharama kubwa na ni rahisi kumuacha kwani tayari anajua kuwa una mtu. Nirahisi kumshawishi mpenzi wa zamani kwakua anakujua na anajua anachoenda kukipata.
Lakini kuna suala kuwa hata kama nikimtaka akikataa sitaumia kwakua nilishamuacha. Kwahiyo Dada yangu kabla ya kupiga simu na kujishaua kuwa unapendwa wewe unapaswa kukumbuka kuwa huo si upendo wewe ndiyo mrahisi rahisi kati ya ma X wake. Usikubali kutumika, hembu itambue thamani yako na jifunze kusema hapana, acha kuwa rahisi kiasi hicho alishakuacha angekua anakuependa angekuoa wewe!
0 Maoni