KOSA LA KWANZA UNAPOTONGOZWA NI KUSEMA HUTAKI KUCHEZEWA!


wa kukuletea furaha.

Wadada wengi wakishaumizwa sana kwenye mahusiano wanakua na hii kauli “Nimeshaumizwa sana kwenye mahusiano sasa hivi natama mtu siriasi sitaki mtu wakunichezea!” Hili ni kosa na mara nyingi ukishamuambia mwanaume hivyo basi unaishi kuchezewa na kuachwa! Najua umeumizwa lakini hembu angalia hizi sababu!
(1) Huyo mwanaume naye kaumiza wanawake wengine hivyo hivyo; Wengi wanaoongea hivyo wana umri mkubwa, kuanzia miaka 28-kuendelea, na wengine wana watoto. Wanataka mwanaume mtu mzima kuanzia miaka 30-kuendelea. Hivi unafikiri kabla yako hakua na mwanamke, unafikiri alipomuacha hakumuumiza huyo mwanamke?
Alikua na mwanamke, inawezekana kamuacha na watoto, kaumiza sana hivyo unapomlalamikia anakuona kama kituko tu kwani ana mwanamke mwingine ambaye kila siku anampigia simu na kumlaani kwa kumharibia maishayake. Kwa maana hiyo hata hatajali, wewe cha kufanya ingia kwenye mahusoano acha kutaka kuonewa huruma.
(2) Mnakua na haraka sana; Wanawake wanaoanza hivyo wanaachika mapema kwakua wanakua na haraka sana, umevumilia ujinga miaka sita kwa mwanaume tofauti, umeachika na makovu yako. Unakuja kwangu unataka nikuoe ndani ya miezi miwili hata sijakujua vizuri, sijakupenda na sijakufurahia kwakua tu ulishaumizwa huko nyuma.
Humpi mwanaume akujue, unaanza masharti mengi mengi, sitaki hiki, sitaki kile, unakuja lini kwetu linakua swali la kila siku. Wanawake wanamna hii wanashindwa kujua kuwa, hata wanaume wanahitaji kuwachunguza ili kujua kama wanafaa kuoa au ni kupoteza muda tui, sasa mtu hata hajakuchunguza miezi miwili sita unataka akuoe kwakua tu ulishaumizwa.
(3) Mnaboa haraka kwakua mnakua na visirani vingi; Wanawake wa namna hii wanakua na visirani vya namka mbili. Kwanza kabisa ni kisirani cha haraka, kila dakika utasikia kwetu unakuja lini, kama haupo siriasi usinipotezee muda wangu, nataka kuwajua ndugu zako na mambo kibao. Mwanaume anaona kama analazimishiwa, kana kwamba kuna tabia mbaya mwanamke anaficha ili ziionekane aolewe tu!
Kisirani cha pili ni cha X, kwamba kwakua walishaumizwa basi kila kitu ambacho mwanaume anafanya analinganisha na X wake, flani naye alianza hivi, flani ilikua hivi flani vile. Hata kama hasemi lakini kichwani anakua na uoga, anakua na hasira za X wake anamshushia mwanaume wasasa, hata kwa makosa madogo atanuna wiki kumbe hakununii wewe anamnunia X wake!
(4) USGAURI WANGU; Unapoingia kwenye mahusiano mapya acha kutangaza kama uliachwa, hakuna mtu anapenda mwanamke wa kuachwaachwa, kulalamika lalamika, unakua kama kiporo na itakua ngumu kwa mwanaume kudili na wewe. Hata kama ni kweli hutataka kupoteza muda mwingi na huyo mwanaume lakini mpime kimya kimya, cha kulazimishia mambo,a cha kubeba maumivu ya zamani na kuyafanya kuwa ya sasa.
Ni kweli umri umeenda, ni kweli una mtoto, ni kweli uliumizwa sana, lakini kwanza si huyo aliyekuumiza na pili kulakamika hakusiadii, sanasana kunakufanya kuwa mtu mwenye kisirani tu na si mpenzi. Unakua unamboa kwakua mwanaume anataka kuoa mwanamke ambaye atampa furaha na si mtu mwenye kisirani! Jifunze kuwa na furaha yako mwenyewe hakuna mtu wa kukuletea furaha.

Chapisha Maoni

0 Maoni