
KAMA UKO MBALI NA MPENZI WAKO ZINGATIA HAYA!
Kama unaishi mbali na mpenzi wako kwanza kabisa unatakiwa kukubali kua mko mbali, huwezi na wala hutakiwi kucontrol kile anachokifanya kule, acha kufuatilia anafanya nini huko, yuko na nani na mambo kama hayo, kwa kfuupi wivu weka pembeni kwani ukiendekeza utachanganyikiwa. Kuna mambo mengi atayafanya mazuri na mabaya lakini kama hakuonyeshei basi huna haja ya kuyafukunyua.
Jambo la pili ni mawasiliano haya ni muhimu na anapokupigia simu au unapompigia tumieni muda wenu vizuri kwa kuongelea kuhusu mapenzi na si kila siku “Mbona hukupokea simu yangu? Mbona nilikuona online hukujibu SMS zangu? Kulalamika sijui nimesikia hivi? Nimesikia vile!” Atakuvumilia kwa muda kisha itaboa na atakua anakwepa kuzungumza nawe na mwisho mapenzi yatakufa.
Hata kama mnaongea dakika tano zifanyeni ziwe tamu zihusu mapenzi na si kuzozana mpaka mtu akitaka kupiga simu anawaza hivi nikiongea naye si kelele tu, hakuna mtu anapenda kupigia simu mtu aliyenuna. Lakini mnapotembeleana hembu dili na mambo yako, sio unafika na kuanza kuchunguza majirani, kuchunguza nani anaingia nani anatoka.
Kuanza kutafuta umbea na vitu kama hivyo, labda kama unataka kumuacha lakini kama bado unampenda basi hayakuhusu sanasana kama humuamini sana muambie mkapime kabla ya chochote ila tofauti na hapo ukitaka kuchunguza utakuta unawachukia majirani, wafanyakazi wenzake na hata marafiki kwani watakua na ukaribu ambao watu watadhani ni wapenzi.
Hata kama mtu anakupenda vipi, hata kama ni muaminifu namna gani lakini kama ukitilia shaka kila kitu basi jua kuwa ndiyo mwanzo wa kuharibu mapenzi yenu. Mnapokua mbali mnakua hamna muda wa kuonana kila saa hivyo zile dakika mnazoongea na zile siku mbili tatu mnazokutana ukizitumia vizuri basi hata kama alikua na madudu yake atakua akifurahia kuongea na kukutana na wewe.
ttps://www.facebook.com/allaboutrelationshipandlife/
0 Maoni