WADADA

WADADA
.
.
Sisiters please naomba mjifunzekuwa na matarajio yanayoweza kutimilika (realistic expectations) kutoka kwa wanaume. Sio vibaya kuwaza makubwa, lakini, hayo makubwa yaendane na jitihada binafsi.
Hii tabia ya kusema, nahitaji mwanaume mwenye gari, wakati wewe unatembea kwa miguu, nahitaji mwanaume mwenye pesa, wakati wewe huna pesa, nahitaji mwanaume mwenye mvuto, wakati wewe bila make up hauna mvuto, nahitaji mwanaume mwenye degrees, wakati wewe hata cheti cha Zoom Polytechnic hauna, nataka mwanaume ambae atani-spoil na mazawadi, wakati wewe ni mbahiri hata kumnunulia boxer ya tsh elfu tano shida..nataka. nataka..nataka... Usihitaji kitu kutoka kwa mwanaume wakati wewe huna jitihada zozote. Hebu timiza yale unayoyaweza kabla ya kuyahitaji kutoka kwa mwanaume. Kwanini ujihisi unahitaji makubwa makubwa kutoka kwa mwanaume kwa vile wewe ni mwanamke? Kwanini usijifunze kutafuta vyako ili akukute ukiwa navyo ili muunganishe nguvu pamoja? Ninaamini mnaweza. Wanaume siku hizi huwa wanawakimbia kiaina wanawake omba omba .
SIYO LAZIMA UNIELEWE ILA UKIWEZA NAOMBA UNIELEWE ITAKUSAIDIA
Share

https://www.facebook.com/allaboutrelationshipandlife/

Chapisha Maoni

0 Maoni