Ila hii ilikuwa tofauti kwa mwanamke mmoja, alikuwa akikaribia kufunga ndoa na mwanaume alie dumu nae ktk urafiki kwa miaka sita, baada ya maandalizi ya muda mrefu sasa walikuwa wakisubiri ile siku muhimu.
Ilikuwa ni siku moja kabla ya harusi yake, ndipo alipopokea simu na kupata taarifa kwamba mume wake mtarajiwa, kipenzi chake amefariki kwa ajali ya gari wakiwemo na shemeji zake waliojeruhiwa
Mwanamke alizimia baada ya kupata taarifa zile, hata alipozinduka alichokua akikizungumza ni kuulizia aliko mume wake kwani hakuamini kama kweli amefariki. Yuko wapi mume wangu, yuko wapi Jay wangu, yuko wapi Jay wangu!! Haiwezekani aniache hivi...nitamfuata aliko!
Na hivyo ndivyo sherehe yake ya ndoa ilivyogeuka na kuwa msiba mzito!
__________________________
Nachukua nafasi hii kukuombea wewe rafiki yangu unaenisoma kila siku katika ukurusa huu, kwamba hila za mwovu shetani zisikaribie upande wako. Muda wa furaha usigeuke kuwa huzuni kwako. Lengo la Mungu likatimizwe kwako. Hutakufa bali utaishi, uishuhudie ile kweli ya Mungu wetu aliye mkuu.
Kama una amini Tushirikiane pamoja kusema 'AMEN
https://www.facebook.com/allaboutrelationshipandlife/
0 Maoni