Mwanangu, nataka niwe mkweli kwako na sitakuficha jambo.
Usiwaze kuhusu ukubwa wa matako au maziwa ya mwanamke, bali angalia ukubwa wa moyo wake na akili yake. Angalia ukubwa wa upendo wake na ustahmilivu wake. Kwa sababu baada ya miaka 5 au 10, haitakuwa kuhusu maziwa yake au matako yake.
Mtazame mama yako, kwa sasa kifua chake kimelala na hata matako yake yanakaribia kunyooka lakini bado tunaishi pamoja kwa furaha, bado nampenda, na yeye bado ananipenda.
Kuwa makini na mwanamke anayependa pesa. Namaanisha mwanamke ambaye 'muda wote' huzungumzia kuhusu nywele zake, nguo, viatu, matoleo mapya ya mikoba na kujiremba tu. Ndoa haijengwi na vitu hivi tu. Bila mapambo, nguo, mikoba, bado ndoa nzuri itadumu lakini hakuna ndoa inayoweza kudumu bila upendo.
Nilipomuoa mama yako, sikuwa na gari wala nyumba yangu mwenyewe. Sikuwa hata na elimu. Lakini nilikuwa na ndoto, na yeye alizitambua na kuniunga mkono. Mwanamke yeyote asiyeunga mkono ndoto zako hafai kufikiriwa hata kwa dakika moja. Kuna wanawake wenye uwezo wa kuziona ndoto zako kuliko hata wewe mwenyewe, ukimpata huyo utakuwa mwenye bahati sana.
Mwanangu, fungua masikio yako vizuri, kuna wanawake unaotakiwa kuwaepuka, usifanye kosa kuwaoa, vinginevyo utajutia. Namaanisha mwanamke ambaye muda wote ana mambo mabaya ya kumzungumzia kila mtu. Ukimuona mwanamke wa aina hii, kimbia.
Mwanamke mbaya kabisa ni yule anayelalamikia kila kitu. Ukinunua hiki atasema ungenunua kile, ukifanya hiki atasema ungefanya kile. Tafadhali kaa naye mbali!
Wanawake wanapenda na wanafurahia kuongea lakini yule anayeongea masaa mawili na kukusikiliza kwa dakika mbili huyo ni 'bomu' kubwa. Kuwa makini naye.
Jihadhari na mwanamke msanii. Mwanamke msanii sio vigumu kumjua. Daima yeye anajua kila kitu kuhusu kila kitu. Funga macho yako na ufungue moyo wako, utaona!
Hakuna mwanamke mkamilifu. Ukimuona mwanamke anayeziamini ndoto zako, anayekuheshimu na kukutii, anayekulindia mali yako na heshima yako, na asiyekuwa mbinafsi, usimuache. Lakini kumbuka, usiwe mwanaume fedhuli, nimeshakufunza!
Ukimpata mwanamke mwema lakini wewe ukawa mwanaume mbaya, hutokuwa na ndoa njema!
Sitakuchagulia mke lakini nimekupatia ushauri wangu. Ukimpata mlete ili nimpe baraka zangu.
Nakuombea upate mwanamke atakayekufanya kuwa mtu bora, sio yule atakayekufanya kuwa mtu duni.

0 Maoni