
Labda nianze kwa kusema kua kweli SMS ni moja kati ya vitu ambavyo vinaleta shida kujibu au kuandika meseji naona kama inachukua muda na inaboa flani hivi ni bora kumpigia mtu simu na kuongea naye mkamalizana, mkajibishana kuliko kukaa kuandika. ♠♠♠Lakini kama mwanaume inabidi ujue kua ni wajibu wako kwa mpenzi wako kufanya hivyo. Katika ulimwengu wa sasa meseji ni sawa na barua. Kwa wale wa kizazi cha kwetu najua mnakumbuka zile barua ambazo zinaandikwa katika karatasi maalum, kubandikwa stika na dedication kibao. ♠♠♠Ndiyo katika mapenzi ni muhimu sana kuandika meseji hasa kwa mwanamke, hii ni kwasababu simu na kuongea thamani yake huisha baada tu ya kukata simu. Kwamba hata kama ulimuambia maneno matamu kiasi gani lakini ukishakata simu basi yanaishia na kule kukumbuka kupendwa kunapotea. ♠♠♠Lakini kwa mwanamke anayekupenda, kunafika wakati akiwa yuko bored, hana kitu cha kufanya au ni mpenzi tu, kuna kitu anawaza na hawezi kuongea nawewe, au anaweza lakini hataki basi atachukua simu yake na kuanza kupitia meseji zako tamu. Hii ni kama zamani ambapo mtu huamua kuangalia ♠♠♠Sasa kama mwanaume nilazima kumpa mpenzi wako kitu cha kukumbuka kama akiwa bored na wewe hupatikani au hataki tu kuongea na wewe. Asome acheke na kukumbuka kua kumbe namimi napendwa. Muandikie mkeo au mepenzi wako meseji za kimahaba, mkumbushe unvayompenda na andika hata upuuzi upuuzi. ♠♠♠Andika kitu ambacho atatamani kukisoma mara kwa mara, acha kua mtu wa kutumiwa meseji tu, kujibu kimkato mkato, mara ok, poa, K na madudu madudu mengine. Hembu bila nini wala nini mtumie meseji, muambie leo nimemisi ile underwear yako unakukaaga namna gflani, ivae basi, muambie namna ambavyo unamkumbuka, mkumbushe sehemu mlipokutana. ♠♠♠Upo sehemu, kuna tukio mlifanya, hembu muambie “Nipo Moro, unakumbuka siku ile tulipo miss kwenda sehemu, unakumbukka tulipochelewa kipindi, unakumbuka siku ile niliposhindwa kupila bili. Yes anza kumtext wewe, muulize hali yake, muambie unavyojisikia, andika SMS ndefu ya kuboa kabisa lakini ataisoma baadaye. ♠♠Ndiyo SMS siku hizi nikama zile barua za karatasi maalum na stika
0 Maoni