UKWELI KUHUSU CHANGAMOTO YA USALITI KATI YA MWANAUME NA MWANAMKE

Image result for USALITI MKUBWA WA MAPENZI
MWANZONI nilidhani ni maneno ambayo yanaweza kuishia vijiweni tu, ila kwa mshtuko mkubwa nikajikuta nikiyasikia hata mbali na hapo.
Hata huko nikaanza kuona mijadala kama ile ya vijiweni ‘eti’ kati ya mwanamke na mwanaume nani anaongoza kwa usaliti. Kila mmoja katika hili anaweza kuwa na jibu lake. Ila kitaalamu kuna jibu sahihi zaidi. Jibu lisilo na chembe ya upendeleo wa upande flani wala uonevu kwa upande mwingine.
Kwanza inabidi kila mmoja aelewe kuwa hakuna jinsia iliyoumbwa kwa ajili ya kufanya usaliti katika mapenzi. Ila usaliti ni suala binafsi linatokana na mmomonyoko binafsi wa maadili. Kwa lugha nyingine ni kwamba, si sahihi kuhusisha usaliti na jinsia yoyote ile.
Katika swali ni nani msaliti kati ya mwanamke na mwanaume jibu ni kwamba hakuna msaliti baina yao. Ila kuna msaliti Juma, Jenifa au Lugito. Sidhani kama utakuwa umenielewa.
Maana yangu ni kwamba, Juma akionekana ni msaliti haina maana kuwa wanaume wote ni wasaliti au Jenifa akionekana mtulivu isiwe kigezo cha kusema wanawake wote ni watulivu. Hapana. Ukiwaza hivyo utakuwa umepotoka sana.
U Usalitili i k kama ili ilivyo k kwa uaminifui if linabaki kuwa ni suala binafsi, lisilofaa kuhusishwa na kundi wala jinsia flani. Ila mbali na ukweli huu pia kuna ukweli mwingine ambao pia nao ni ukweli.
Bila shaka kuna baadhi bado watakuwa na shauku ya kujua kuwa mbali na usaliti kutokuwa suala la kubebeshwa lawama kwa jinsia flani ila ni kundi gani zaidi limeathirka na janga hili?
Kwa mujibu wa takwimu za kitaalamu kundi lililoathirika zaidi na suala hili ni wanawake. Ndiyo, wanawake. Kwanini?
Katika hali ilivyo mwanamke ni mwanadamu anayetongozwa zaidi kwa siku kuliko mwanaume. Kima cha chini cha mwanamke kutongozwa ni kati ya wanaume watatu mpaka watano kwa siku. Ila hiyo pia bado haijawa sababu.
Sababu ya wanawake kuathirika zaidi na suala hili ni kutokana na wengi kati ya wanawake kutokuwa imara katika kupambana na mbinu za wanaume pindi wanapotongozwa. Ikumbukwe tu, idadi ya wanawake ni wengi kuliko wanaume. Kutokana na hali hiyo wanawake wengi huamini kuwa na wanaume wenye mvuto au kipato kikubwa ni bahati kutokana na idadi yao.
Kutokana na kuwa na kitu hicho katika ubongo wanawake wengi walio katika mahusiano wakitokea kutongozwa mara kadhaa na watu wa aina hii huwa si wagumu sana kusema ndiyo, kwa kuwa ni ‘ bahati’ kwao.
Pia sababu nyingine inayofanya kundi la wanawake waonekane kama kuongoza katika kuathirika na tabia hii mbaya ya usaliti ni hali ya kugombana katika mahusiano.
Wanawake wengi wasio na uimara zaidi katika kupambana na changamoto za ndoa, inapotokea wamegombana na wapenzi wao huamini mapenzi yanaelekea mwisho.
Sasa kutokana na hali hii mwanaume anapomfuata na kumtongoza hujikuta akitaka kuandaa mazingira mapema ya kuwa na mpenzi baada ya kuona mapenzi yake ya awali kama yanaanza kufika tamati. Hapo hujikuta akimkubalia akiamini atamfaa baada ya kuachana kabisa na aliye naye. Sasa hapo mwanamke husika hujikuta njia panda baada ya ugomvi wake wa awali na mwenzake kutatulika.
Hapo huanza kuwa mjanja zaidi kutaka kutimiza haja za wote wawili ili kila mmoja ajihisi yuko mahala salama. Hapa mwanamke huwa na hali ngumu zaidi kutokana na mara nyingi wakati anatongozwa na yule mwanaume wa pili husema hana mtu, akiwa na matumaini mapenzi yake na mpenzi wake wa awali ni lazima tu yavunjike. Mbinu nyingi za kisaliti huwa zinatumika sana hapa ili kuweka hali katika usawa anaodhani ni bora.
Pia hali ya kutoridhishwa katika mahusiano pia huchangia kwa asilimia kubwa wanawake kuongoza katika suala la usaliti. Ni idadi ndogo sana ya wanawake wanaokatwa kiu na wanaume wao katika kufanya nao mapenzi ukilinganisha na idadi ya wanawake waliopo katika mahusiano.
Ni asilimia ishirini na tano tu ya wanawake ndio huwa wanafurahishwa na wenza wao wakati wa kufanya mapenzi ila wengi wao huachwa njiani na kiu yao.
Kutokana na hali hiyo kuwa ya kukera na kuumiza, wanawake wengi hujikuta wakishindwa kuvumilia na kuamua kutafuta tiba katika hospitali nyingine.
Hapo ndipo flani anapoanza kunyooshewa kidole kuwa ni msaliti na hafai katika jamii ya wastaarabu. Kwa asilimia kubwa hili tatizo limeongeza usaliti mwingi katika mahusiano. Tabia ya wanaume wengi kujiangalia wao tu katika suala la kuridhika katika tendo la ndoa limefanya wanawake wengi watoke nje .
Wanaume wachache ndio wenye kujua kuwa mwanamke anahitaji maandalizi ya muda mrefu sana kabla ya kuanza kushirki tendo. Wengi hawaangalii hilo. Wao wakijiona wako tayari ‘huwavamia’ wake zao na shughuli huanzia hapo. Na matokeo yake hujikuta ni yeye tu akifurahia tendo huku akimuacha mwenzake akiwa bado ana njaa ya safari.
Sababu ziko nyingi sana na ipo siku nitaziorodhesha na kuzichambua kwa kina. Kwa leo tuseme inatosha.

Chapisha Maoni

0 Maoni