Kijana mmoja alikuwa anafanya kazi jeshini huku akifedheheshwa mara kwa mara kwa sababu alimwamini MUNGU.
Siku moja Kapteni alitaka kumfedhehesha mbele ya Askari wengine.
Basi alimwita yule kijana kisha akasema;
"Wee kijana kuja hapa, chukua hii funguo nenda ukapaki ile Jeep kimvilini"
Kijana kwa upole akajibu; "Siwezi kuendesha gari mimi MKUU!" Kapteni akasema; "Naammh! Aya omba msaada sasa kwa MUNGU wako unaye muombaga! Atuonyeshe kuwa yupo!" Kijana kwa unyonge akachukua ile funguo, akaelekea lilipokuwa ile gari akapiga magoti nakuanza kuomba.
" Eh MUNGU najua unajua kuwa hawa watu wahaitaji kuona uwepo wako, basi nakuomba uonekane maana wewe ni dereva mwema. Naamini juu ya ili hawa watu watabadilika." Akaingia kwenye ile jeep akaliwasha likawaka nakulipaki mahali alipoelekezwa vizuri kabisa na kikamilifu kama kapteni alivyotaka.
Kijana akatoka nje ya jeep ajabu aliwaona wanajeshi wenzake wote wakilia.!! Wakasema kwa pamoja;
"Tunataka kumtumikia MUNGU wako!" Yule Askari kijana akastaajabu sana kisha akawauliza; "Nini kinachoendelea, mpaka wanalia?" Kapteni huku akilia kama mtoto akafungua boneti ya ile Jeep na kumwonyesha kijana kwamba gari haikuwa na injini. Ila alikuwa akimkejeli tu sababu anajua kuwa hawezi kuendesha gari na hakuna MUNGU wakuweza kuifanya iyo Jeep itembee bila injini.
Kijana kuona hivyo akasema; "Umeona eh? Huyu ndiye MUNGU ninayemtumikia;
MUNGU anayekupa uhai kwa kile kisichokuwa na uhai kabisa.
MUNGU aliye pasua Bahari ya shamu waisrael wakavuka.
Hakika huyu ni MUNGU WA YASIYOWEZEKANA." UJUMBE:
Unaweza kufikiri kuna mambo hayawezekani lakini kwa MUNGU kila kitu kinawezekana. HAKUNA LISILOWEZEKANA KWA MUNGU!
Kwa wewe unayesoma hii, Andika 'AMINA' au 'AMENumuombe choxhote ukiwa na imani kuwa MUNGU atatenda.
@
0 Maoni