Mapenzi yanauma, mtu ulikua unampenda sana.



Mapenzi yanauma, mtu ulikua unampenda sana. Ukajitoa kwake ukawa muaminifu, umewekeza muda, pesa na mwili wako kwake, ulishakuwa na mipango mingi na yeye.

Umevumilia mengi, upuuzi wake, maisha yake magumu, umekuwa mwema katika vipindi ambavyo mambo yalikuwa magumu, hukuwahi kumsailiti na wala hukuwahi hata kufikiria kumsaliti.

Lakini ghafla, bila sababu yoyote anaanza kukudharau, kukudhalilisha na kukunyanyasa, huchoki unavumilia, amekufanyia mengi lakini bado unajipa moyo kuwa atabadilika hivyo utavumilia.

Lakini anaona kuwa hutaki kumuacha pamoja na vituko vyake, anakuacha bila sababu, au anakupa sababu ya kipuuzi kabisa. Unaumia, unalia, uanchanganyikiwa, ukiangalia muda wako na mambo yaliyokupita kwasababu yake unachanganyikiwa.

Ghafla unaona unataki waulipe kisasi, unajiona mpuuzi kwakua ulivumilia lakini ukatendwa, unaanza kuwaza sasa kwanini uwe muaminifu wakati ulishakuwa muaminifu na bado ukatendwa.

Unaamua kuwa kicheche kama yeye, unaamua kufanya mambo yote ya ajabu ajabu ambayo awali ulijizuia kwaajili yake, kichwani unafikiri unamkomoa, unafikiri labda anaumia, unatemba na rafiki zake wote.

Huishii hapo hata kwa ndugu zake, unataka kumchoma. Lakini mpaka unastuka yeye kaoa au kuolewa, kumbe alishakusahau siku ya kwanza tu alipokuacha, ujinga wote ulioufanya unakuwa hauna maana.

Unakuharibia jina, unafanya watu wanakuchukia na wewe mwenyewe unajichukia, unajiona tena huna thamani. Ndugu yangu maisha ndivyo yalivyo, kuna kuumia na kuumizwa, lakini kuna kupjipanga na kukutana na mapya tena.

Hembua acha kuoga na ndoo ya mavi kwakua ulikanyaga kinyesi. Huyo mwenza wako alikuwa ni kinyesi, ulimkanyaga kwa bahati mbaya kwakua ulikua hujui, ulikuwa unaamini ni salama lakini sasa umemkanyaga na inabidi ukaoshe mguu.

Unanuka kinyesi kidogo, lakini dawa ya kukanyaga kinyesi ni kunawa au kuoga, si kwenda kuchukua ndoo ya mavi na kunyimwagia. Kwamba ukasema kuwa eti kwakua ushaumizwa, ushakutana na vicheche na wewe uwe kicheche.

Nakuambia, utakoga na kinyesi hutamkomoa mtu, utajikomoa wewe, kwani harufu yote utaisikia wewe, lakini mbaya zaidi yule ambaye ulitegemea aisikie harufu na yeye akasirike atakimbia na kuondoka.

Chapisha Maoni

0 Maoni