Kwa taarifa tu... Wewe MWANAUME



Fanya ujinga wako unavyoweza lakini ukiona mwanamke ameacha kulalamikia mambo ambayo zamani ilikuwa ni kelele kubwa kati yenu basi jua kuwa kuna mambo mawili. Jambo la kwanza inawezekana kuwa kashaanza kukuchoka na hajali tena na inawezekana ana mtu mwingine ambaye anampa amani, hata kama huyo mtu anajua hawawezi kuwa pamoja lakini angalau anafuraha na huyo mtu.

Sababu ya pili ni kwamba huyo mwanamke kashakukatia tamaa kuwa hutabadilika na kaamua kujipa furaha yake mwenyewe. Wala hachepuki, wala hana mpango wa kukuacha, wala hana mpango wa kutafuta mtu mwingine, lakini kakaa kafikiria hivi nahangaika nini? Nitapiga kelele mpaka lini? Nitahangaika na wanawake zake katika mitandao mpaka lini?

Hivi mimi ni mtu gani kila siku kupekua simu yake na kukuta mapicha ya uchi? Hivi huyu mwanaume ni pumzi kwamba nisipohangaika naye nitakufa? Ameacha kuhangaika na wewe na ameamua kujihangaikia. Ameamua kupendeza kwa ajili yake, ameamua kudili na maisha yake, kujifurahisha bila kujali kama umenuna au unaendelea na upuuzi wako!

Mwanamke akishachagua kuwa na furaha yake mwenyewe basi jua kuwa ni zamu yako ya kuteseka, ni zamu yako ya kukagua simu yake, ni zamu yako ya kupiga simu na kutuma meseji miamia kuulizia kuwa yuko wapi? Kama una mwanamke ambaye anakupenda sasa hivi, angalau anakuuiliza kwanini unarudi saa nane basi mpende, mpe hata jibu zuri hata kama ni la uongo lakini acha kumtukana na kumdhalilisha.

Siku akicha kujali utatamani akuulize lakini hatauliza.🚶🏾‍♂🚶🏾‍♂🚶🏾‍♂🚶🏾‍♂
maana ulimgeuza store yako ya kujipakulia tu, ukidhani anakuona kama lulu au dhahabu, hata ukifanya ujinga namba ngapi atakuvumilia
.. Sasa macho yake yameshafunguka.. Na ameshaamua.. Kama kwako alikua akiba basi endelea kumtumia aliyekua chaguo la kwanza kwako na sasa naye anataka awe chagua la kwanza kwa mwingine na atakua maana wewe ndio ulikua kikwazo kikubwa kwake.. .. Dada jikubali nakupa moyo wa nguvu leo..
Wewe wapo wanaokuona na kukuweka kwenye gredi kubwa kwenye mioyo yao wa nakupenda na wanawaza watakupataje na lini ili wakupe furaha ujute kupotezewa muda na hilo dudu mtu

Chapisha Maoni

0 Maoni