Kuna wakati wenza wanaweza kuingia katika mtafaruku ambao chanzo chake ni cha ajabu kabisa!

Related image


Kuna wakati wenza wanaweza kuingia katika mtafaruku ambao chanzo chake ni cha ajabu kabisa! Kwa mfano, unakuta mpenzi anamwambia mwenzake: “Mh! Na wewe unanuka sana mdomo!” Kauli gani hiyo kwa mwenza wako? Mwanaume au mwanamke unalala naye kila siku, kwa nini umwambie ananuka? Wewe ukifanya hivyo, huko nje wamuambieje? Kwanza kama ni kweli ana tatizo hilo, ni jukumu lako kumtibu, lakini pia kumtunzia siri.

Kama nje anachekwa, ndani ya familia pia anachekwa, wapi atapata faraja? Yapo maneno mengi sana yenye kuudhi, lakini hapa nitataja machache. Wengine wanawaambia wenza wao wananuka kikwapa, hawajapendeza, hawana akili nk.

Haya ni maneno ya kuudhi sana. Hebu fikiria kauli kama hii mtu anamtamkia mkewe! “Yaani kweli wewe huna akili, kitu kidogo kama hicho kweli unaweza kukosea? Ndiyo maana wenzetu wanafanikiwa kimaisha, wanatuacha. Sijui nilikutana na wewe wapi?... maisha yangu yanazidi kuwa giza tu, nikiwa na wewe!” Maneno kama haya yanakera na kukatisha tamaa kabisa katika ndoa.

Au una mwambie mmeo "ndio maana hutajiliki, au kwani na wewe ni mwanaume sasa
Hizi kauli hua haziishi akilini mwa mtu, hua zinakaa na kuishi siku mmeo akija kupata pesa ataanza kukulipixa kisasi na visasi vingi hua ni kukuchepukia na kuto kukujali kabisa

Acha maneno ya kufuru, kwani siku zote hukuona upungufu wake? Kuwa makini na kauli zako. Ndoa yako utaivunja wewe mwenyewe, pia kama ni kuijenga, utaijenga wewe mwenyewe. Kuwa na kinywa chenye kuchuja kauli zako kwa mwenza wako

Chapisha Maoni

0 Maoni