KUPENDA PEKEE SIYO MKATABA

Related image

KUPENDANA pekee hakufanyi watu wadumu katika mahusiano, wapo wengi waliopendana ila safari yao ya mapenzi iliishia njiani.

Ili uweze kudumu katika mahusiano yako,  inabidi umjue mwenzako kiuhakika, ujue namna ya kumfanya afurahi na namna ya kumfanya achanganyikiwe kwa sababu yako.

Mwenza wako anaweza kukupenda sana ila kama huwezi kucheza na akili yake kwa namna ya kumfanya azidi kukuona bora na wa thamani, tambua mwingine anaweza kufanya hivyo na kumuondoa kwako.

Mapenzi hayadumishwi na I LOVE YOU pekee ama kushinda naye chumbani muda wote, sehemu yenye nguvu zaidi katika kuimarisha mahusiano yako ni katika kucheza na akili yake na kumfanya akuone wewe ndiye dunia yake.

Unaweza kumhonga sana na bado akaondoka, anaweza kukupenda sana na bado siku moja akaona heri aende.

Ili mapenzi yako yawe imara kwa mwenza wako, hakikisha karibu kila siku anakuwa surprised na wewe katika jambo fulani.

Watu hawadumu kwa sababu wanapendana, wanadumu kwa sababu kuna VIONJO vya kila aina katika mahusiano yao.

@maisha_halisitz
Lipia ushauri ni elfu 10 tu unalipa kwenye voda no 0756802580 then una kuja WhatsApp no 0656832100 jina litakuja la mme wangu emmanuel hosea

Chapisha Maoni

0 Maoni