
Katika mapenzi ni lazima umsome na kumjua mtu wako na kubwa kabisa kujua namna ya kumfurahia hivyo hivyo alivyo. Hili ni kubwa hasa kwa wadada, kuna maswali mengi naulizwa unakuta mtu anakuuliza mpenzi wangu hapendi kuchati? Si mtu wakutoka? Hanisifii? Anahudumia familia lakini mimi hanihudumii? Anajali tu watoto wake lakini mimi hata kuniuliza naendeleaje hawezi?
Zinaweza kuwa ni tabia zinakukare, ungetamani akufanyia kitu flani, lakini kama umeongea mara mbili tatu na habadiliki basi jua kuwa huwezi kumbadilisha. Una mamauzi mawili, kuondoka kwenda kutafuta huyo anayetuma meseji au kukubaliana na ukweli, kuacha kisirani na kuacha kuumizwa na hizo tabia au hivyo vitu ambavyo ungetamania kufanyie.
Kwakua najua huwezi kuondoka basi hembu acha kulalamikia kitu kila siku, ukishaongea mara mbili tatu kama habadiliki basi jua ni tabia yake. Jifunze kuishi naye hivyo hivyo kwa furaha, tofauti na hapo basi kila siku utakua na kisirani, utakua ni mtu wa kulalamika, kununa, kulia na kusononeka. Unajikuta unaishia kuwaonea wivu mashoga zako, kutamani ndoa zao za kuigiza hivyo kutengeneza kisirani zaidi na kuvunja ndoa yako zaidi.
Nilazima ujifunze namna ya kujipa furaha yako wewe mwenyewe, ujifunze namna ya kuacha baadhi ya mambo yapite na kaucha kisirani. Hembu chukua kalam na karatasi, andika mambo matamu anayokufanyia na mambo ambayo hakufanyii. Yale anayokufanyia basi yafurahie na yale ambayo hakufanyi jifunze namna ya kujifanyia mwenyewe au namna ya kuyapuuza na kuyaona yakawaida, huwezi kupata kila kitu katika ndoa, furahia hicho hicho kilichopo.
Mimi nishamaliza hujui namna ya kujipa furaha basi
0 Maoni