ACHA KUJIDHALILISHA KWA KUHANGAIKA NA MICHEPUKO YAKE HAIWEZI KUMBADILISHA MUME WAKO WALA KUKUPA FURAHA!

Related image

ACHA KUJIDHALILISHA KWA KUHANGAIKA NA MICHEPUKO YAKE HAIWEZI KUMBADILISHA MUME WAKO WALA KUKUPA FURAHA!

Mara nyingi wazo la kwanza kwa wanawake wengi wanapowafumania waume zao au hata wapenzi wa kawaida ni kuwasiliana na huyo mwanamke ambaye wanahisi anatembea naye na kumtukana au kumuonya kuachana na mumewe au mpenzi wake. Kwamba umekuta namba ya simu, wanachat na kutumiana mapicha ya ajabu ajabu, badala ya kuongea na kumalizana na mume wako moja kwa moja unaanza kumtafuta huyo mwanamke mwingine.

Unampigia simu, unaweza kumuuliza kistaraabu kua anamfahamu mtu flani, ukamuambia ni mumeo au ukaja kwa ukali ukamtukana na kumuita Malaya ukamtishia na kumfanya ajisikie vibaya. Hii itakufanya ujisikie vizuri kwa muda lakini haitakusaidia chochote zaidi ya kukuongezea matatizo. Kwanza nikua inawezekana huyo mwanamke uliyekua unaongea naye alikua tayari anajua ana mume au mpenzi.

Alishajiandaa kutukanwa na hata hajali, pili hata kama alikua hajui ni wachache sana ambao watakubali kumuacha, tena hawa ni wale walitegemea ndoa au ni waoga sana, wengi kama alikua anafaidi mapenzi tu au pesa hata kama akijua kashaoa hataachana nayeye. Lakini tatu nikua hata huyo uliyemtukana akiachana na mume wako hiyo haimaanishi kua mume wako ataacha kuchepuka hapana, hiyo ni tabia yake ataendelea tu.

Sanasana utakachokua umemsiadia ni kumkimbizia tu huyo mwanamke na yeye ataendelea kutafuta mwingine. Baada ya muda utajikuta wewe una kazi ya kutukana tu michepuko yake kwani ukitukana huu akiachana nao atatafuta mwingine utatukana na kutukana na baada ya muda atakuchoka na hata kukupiga kwani unamletea usumbufu wa bure.
Atakuona kama huna kazi ya kufanya unapoteza muda kutukana wanawake zake tu, hatakuheshimu na ataizdi kuchepuka kwani atajua kuwa hata kaifanya hivyo hutadili nayeye unadili na watu wengine. Hao wanawake wengine walitongozwa kama ulivyotongozwa wewe na kukubali, sio makosa yao kukubali hata kama walijua kaoa, mwenye kosa ni huyo mumeo ndiyo mtu wa kudili naye na kama huwezi basi kaa kimya sio kusumbua watu wengine.

Chapisha Maoni

0 Maoni