
Dada nisamehe tu
Wakati mwingine inatokea, unakuta unaingia kwenye mahusiano na mwanaume wa rafiki yako, mnapendana na anakuchagua wewe. lakini si hivyo tu, unakutana na mwanaume kumbe alikua na mtu wake hata humjui lakini walipendana au hata kama mwanamke alikua anadanganywa lakini walikua pamoja na mwanamke alikua anapenda sana. Sisemi unamchukua kwani mwanaume hachukuliwi bali mwanaume anaamua kuwa na wewe.
Sasa ushampata mwanaume, badala utulie na mwanaume wako kutwa kucha uananza vijembe na kuchambana na X wake, kuchambana na Mama wa mtoto wake au kuchambana na mke wake wa zamani, au pengine hata si mke wake wa zamani bali mke wake wa sasa. Mbali na kwamba ni ushamba, lakini nikuonyesha kuwa hujiamini. Yaani ni kama umempata kwa bahati, ni kama unajiona kinyesi flani hivi na kuona kama ni bahati kuwa na huyo mwanaume kwamba hukustahili.
Kila saa kujifanya unapost ili watu wawaone kuwa mna furaha, kumtag na kuweka status za vijembe ukidhani kama unamkomoa X wake. Labda nikuambie tu, humoi na kama ni kumuumiza basi utamuumiza kwa muda lakini mwanaume akishajua kuwa hujiamini au huamini kama umempata basi jua kuwa ndiyo mwanzo wa manyanyaso. Anaweza kuvumilia vituko vyako kwa muda lakini akishakuzoea ule upya ukipotea kama asiporudi kwa X wake basi ataenda kwingine kwakua ulishamboa kwa uswahili wako.
Iko hivi, karibu kila mwanaume ana X wake, iwe ni X-mpenzi, X-mchumba, X-mke au Xdanga jua yupo. Hivyo kama kakutongoza kakupata wewe basi jua anakutaka wewe, huna haja ya kushindana na ma X wake kuwawekea vijembe, nikuonyesha tu kua hujiamini na muonekano wako na ni uoga ambao utakuja kukugharimu. Kwanini uwe na kisirani na mtu aliyeachwa, wewe si ndiyo umepatwa sasa kuhahahaha kwanini, kaa tulia, wanaume hatupendi hayo mambo.
Kama kila siku unashindana na X wake utamfanya ashindwa kufurahia utamu wako na kuwaza “Mhhh mbona huyu anamuogopa yule hivi sio kama utamu mwingi upo kule?” Huwezi amini, chunguza wadada wengi wa vijembe ambao wanahangaika na ma X wa wanaume zao, hawavuko mwaka washachokwa kwakua tu waslishajiharibia mwanzoni. Hembu jiamini, hujamnyang’anya mtu,
Mwanaume hayang'anwyi.
0 Maoni