NDOA YAKE, KIFO CHAKE. HEART TOUCHING STORY.



NDOA YAKE, KIFO CHAKE. HEART TOUCHING STORY.

Ilikuwa ni Jumamosi tulivu, sikuwa na kazi nyingi sana. Siku hiyo nilikuwa na miadi na mmoja wa wateja ofisini kwangu kituo cha msaada wa Kisaikolojia HT&L CLINICAL THERAPY.

Mteja wangu alikuwa akiitwa Claudia (sio jina lake halisi). Alikuja kwangu na kulalamika ni kwa jinsi gani amegundua kuwa mumewe sio muaminifu na anatoka nje ya ndoa.

Alikuwa anahisi kusalitiwa mno na alikuwa amechanganyikiwa, alikuwa akinielezea hali jinsi ilivyo huku akitokwa na machozi. Nilijitahidi kumpa moyo na kumueleza kuwa haya yataisha.

Nikamuomba anipe namba ya simu ya mumewe na nikamuahidi kukutana na wote, yeye na mumewe tuweze kupata suruhisho la matatizo ya ndoa yao. Pia nikamhakikishia kwamba kwa Neema ya Mwenyezi Mungu amani itarudi ndani ya ndoa yao.

Baada ya wiki moja niliweza kuwasiliana na mumewe na hakuwa mkaidi alikuja ofisini kwangu na tukawa na 'session' pamoja yeye pamoja na mkewe. Baada ya maongezi ya kirafiki, alikubali kwamba ni kweli anao mchepuko. Na amekuwa akichepuka mara kwa mara.

Alimtupia lawama zote mkewe na kuniambia kwamba haya yote mpaka yeye kuchepuka nje na kutojali ndoa yake amesababisha mke wake mwenyewe.

Akaniambia matatizo yalianza pale dada wa mke wake yaani shemeji yake alipokuja kuishi nao. Walikuwa na ndoa changa ndio kwanza ikikuwa. Kwa maneno yake alinisimulia;

" Tulikuwa tumepanga chumba kimoja tu, na niliona si vema huyu shemeji yangu nae awepo kwenye chumba kidogo kama kile"

"Tulikua tunahitaji muda mrefu kidogo tukiwa peke yetu ili kujenga ndoa yetu changa bila kuingiliwa na ndugu au mtu yeyote, hivyo dada wa mke wangu alitunyima kabisa uhuru wa mimi na mke wangu kuwa pamoja"

"Shemeji yangu, yaani dada yake na mke wangu alikuwa anao uhuru wa kupitiliza, aliingia tunakolala na mke wangu, alikuwa akilala kitanda chetu muda wowote anapojisikia na alikuwa haniheshimu hata kidogo hata mbele ya mdogo wake"

"Na kila nilipokua nikimueleza mke wangu juu ya tabia za dada yake na kumsisitizia amwambie arudi kwao, mke wangu alinijia juu na kuniambia nina mdharau ndugu yake, na kama anataka aondoke basi na yeye ataondoka"

"Nilichanganyikiwa kwa kweli, shemeji yangu alikuwa na kiburi, kila nikimueleza arudi nyumbani kwao hakunisikia, nilishangaa mno kwa nini alikua aking'ang'ania kukaa nasi kwenye chumba kimoja na huku ndoa yetu ikiwa ndio kwanza ipo changa"

"Mara ya mwisho mimi kumgusia hilo suala, ilikuwa ni siku ambayo mke wangu aliniambia mbele ya dada yake kwamba dada yake hataenda sehemu yoyote. Sikuweza kuvumilia, ukizingatia nilikuwa nimekaa kama miezi miwili hivi bila kushiriki tendo la ndoa."

Sikuweza kuvumilia kwa kweli, nilivaa viatu vyangu nikatoka. Sikuwa na uelekeo maalumu, nilizunguka zunguka tu mpaka nikafika Bar fulani iliyo nje ya mji kdogo. Nilikaa katika hiyo Bar nakuanza kunywa bia, pembeni yangu alikaa dada mmoja ambae alikuwa mrembo kweli"

"Nilimkaribisha mezani kwangu, tulikunywa sana bia pamoja na baadae nikachukua chumba pale pale maana Bar ilikuwa na vyumba pia. Niliingia nae na nikafanya nae mapenzi"

"Na hapo ndipo nilipoanza kuchepuka, yule dada niliyekuatana nae pale Bar alikuwa akiitwa Diana (sio jina lake halisi). Na alikuwa akiishi bagamoyo. Tukatokea kupendana sana. Nikawa nikisafiri kwenda Bagamoyo. Mara nyingi nilichelewa kurudi nyumbani au siku nyingine nikawa sirudi hata siku mbili tatu hata wiki" Mume wa yule dada alinipa hayo maelezo yake.

Kwa kufupisha story, baada ya kumsikiliza huyu mume japo mke alikuwa amepanick, mimi niliongea nao maongezi ya kina, niliwaonesha maandiko ya Mwenyezi Mungu yanasema nini juu ya Ndoa na nikawaeleza hasara za yeye mume kuendelea kuchepuka, huku akiacha mkewe wa ndoa. Pia nikampa mbinu za kufanya ili shemeji yake aweze kuondoka pale nyumbani kwake.

Mke nae nilimueleza umuhimu wa mume wake hasa kipindi hiki ndoa ikiwa bado changa na ikihitaji jitihada za wote wawili. Na kumsisitizia aruhusu dada yake aondoke.

Walinielewa na nilifurahi kwa kuwa mume aliniahidi kurudi kwa mkewe na kuendeleza ndoa yao changa.

Ndugu msomaji, kama mchekeshaji maarufu hapa Tanzania Mjuni Mpoki alivyoimba katika kibao chake kimoja kwamba "Mapenzi yana nguvu kuliko hata breakdown." msemo huo ulijidhihirisha kwani yule mume, baada ya kukaa siku chache tu na mke wake alirudi Bagamoyo kwa mchepuko wake, ingawa shemeji yake yaani dada wa mkewe aliondoka na kuwaachia uhuru.

NA NDIPO JANGA LILIPOTOKEA!

Usiku mmoja mkewe ambae alikuwa na pumu (asthma) akiwa peke yake, wakati bwana mkubwa yupo kwa mchepuko wake Bagamoyo, pumu ilimbana sana, Blood pressure (BP) ililuwa juu, sauti haikuwa inamtoka, alihangaika sana na mwishoe akafariki kutokana na hiyo attack (shinikizo)

Ndio alifariki kifo cha maumivu mno pasina msaada wowote, aheri hata angalikuwepo mtu yeyote ndani huenda angaliweza kutoa msaada wa haraka wa kumuwahisha hospitali!

_________

Sote tunapaswa tujifunze kuweka ndoa zetu au mahusiano yetu mstari wa mbele, panapokuwa na mapenzi ya kweli na heshima kwa kila mmoja wetu, hali kama hiyo hapo juu haiwezi kujitokeza na hata ikitokea basi huamuliwa kwa busara na matokeo hua ni chanya. Sio hasi kama yaliyotokea katika simulizi hapo juu.

Sasa tusemeje?

- Je Mwanamke alijisababishia kifo chake mwenyewe?

- Mume wake ndio alikuwa chanzo cha kifo chake?

- Ni kweli mke wake alipaswa kulaumiwa kwa yeye kuanza kuchepuka?

- Au tumlaumu dada mtu kuja kukaa kwa shemeji yake na huku akijua wanaishi chumba kimoja tu?

Toa maoni yako hapo chini.

Ndoa sio mchezo, ndoa sio masihara, if you mess up with marriage it might be the way to your grave. Be wise and pray to God.

https://www.facebook.com/allaboutrelationshipandlife/

Chapisha Maoni

0 Maoni