Aliyomweleza Mke Wake



Aliyomweleza mke wake.......

Mpendwa mke wangu, hivi ni vitu vitatu ninavyopenda uvijue kuhusu mwili wako.

Hivi karibuni nimegundua kwamba umekuwa ukihangaika sana kuhusu mwonekano wa mwili wako. Sijajua kwa nini, kwa sababu kiukweli mimi nafikiri uko sawa kabisa.

Kama mume wako kuna vitu vitatu nataka uvijue kuhusu mwili wako;

1. Wewe ni Mzuri.

Haina haja ya mimi kuzunguka msitu, niwe mkweli kwako moja kwa moja. Wewe ni mzuri nadhani hujasahau hilo, ninavutiwa sana na wewe na ninahitaji kuwa na wewe siku zote.

Ndio tunaendana, naweza nisiseme mara kwa mara kile ninachohisi juu yako, ila mara nyingi najiambia mwenyewe nafsini mwangu jinsi gani ulivyo mzuri na jinsi nilivyo na bahati kuushinda moyo wako na kuwa mume wako.

2. Nakupenda jinsi ulivyo na unavyojitahidi kujitunza. Nafsini mwangu najua unafanya hivyo kuzidi kunivutia mume wako, sijui kama nawaza visivyo. Napenda tunavyotoka "out" wote, najiona nina bahati ya kuwa na mwanamke kama wewe pembeni yangu.

Ila kuna kitu kimoja cha msingi nataka ukijue. Nakupenda jinsi ulivyo! Katika dunia ya sasa wanawake wengi wamekuwa hawajiamini, wamekuwa wakitumia vipodozi vikali kujichubua ngozi zao wakisaka weupe na kuukana weusi. Ila kwako sijaliona hilo na hii inanifanya nizidi kukupenda zaidi jinsi ulivyo "natural"

Nakupenda jinsi ulivyo!

3. Tabasamu lako linaleta mwanga ndani ya nyumba. Tumekuwa katika ndoa kwa muda sasa, ninapenda sana kukushika mikono na kuwa karibu na wewe. Ila nataka nikukumbushe kwamba kabla hatujaingia katika Ndoa, tabasamu lako lilikuwa likinivutia mno, ni bahati kwamba tabasamu lile lile la kipindi kile unalionesha mpaka leo hii.

Tabasamu lako ni zuri mno, huleta mwanga ndani ya hii nyumba yetu kama vile ulivyoleta mwanga katika maisha yangu, mpaka hivi sasa nimegundua kuwa kukuoa wewe ulikuwa ni uamuzi wa busara ambao sijawahi kuufanya!

Hivyo basi mke wangu mpenzi, pamoja na stress na pressure za ulimwengu huu, usiache mwili wako uharibike, kula vizuri, usipendelee vyakula vyenye mafuta, vyakula vya sukari nyingi na juice za viwandani zitumie kwa kiasi, pia jitahidi kufanya mazoezi mepesi, endelea kujitunza nami nitaonesha jitihada zangu katika kukufanya uzidi kunivutia.

Ingawa naweza nisikueleze haya mara kwa mara, tambua tu wewe ni mzuri, asante sana kwa kuwa kila kitu kwangu, asante kwa kunilelea watoto wangu!

Nakupenda mke wangu, nakupenda pambo langu!


https://www.facebook.com/allaboutrelationshipandlife/

Chapisha Maoni

0 Maoni