NGOJA NIKUPE TAARIFA TU KAMA ULIMCHEZEA NA SASA YUPO KIMYA. HUONI SMS WALA CALLS :-Nikwamba


Kwa muda mrefu sana amejitahidi kukuonesha kwamba anakufaa lakini alichoambulia ni maumivu. Hatimae moyo wake umechoka, hatakutafuta tena. Hatimae amejikuta hana ujasiri tena wa kukunyenyekea.
.
Hatimae amejiona hawezi tena kukupigania. Kila kosa ulilolifanya limemuweka katika mazingira ya kutokukuamini tena. Maumivu uliyomsababishia yamemfanya aamini wewe ni mbaya kwake.
.
Hivyo, usiamini kama atarudi tena. Usitegemee kabisa kuwa atarejea tena na kulilia kupendwa na wewe. Usitarajie atarudi ili azidi kuumia kila siku kama hapo awali.
.
Imemchukua muda wake mwingi kujiamini na kusema kwamba "imetosha sasa", imemchukua muda mrefu kuamini kuwa ataweza ku-move on. Lakini sasa amefanikiwa na hakika hatarudi tena nyuma.
.
Ndio. Itakuwa ni ngumu kwake kwakuwa ameshakuzoea. Itakuwa ngumu kuwa peke yake tena. Lakini bora awe peke yake kuliko kuwa na mtu ambaye hakuna uhakika wa kufika nae popote.
.
Ndio, itakuwa ni ngumu kumpenda mtu mwingine tena, lakini ni heri. Maana, atapenda tena pale atakapokuwa tayari kuliko aendelee kumpenda mtu anayemchukulia poa. "Letting go doesn’t mean that you don’t care about someone anymore. It’s just realizing that the only person you really have control over is yourself.
NATAMANI UMU TAG ILA NO UTAMPA KIKI😅😅
tell him/her alikua kikwazo and now una barikiwa daily
Wenu kazini

https://www.facebook.com/allaboutrelationshipandlife/

Chapisha Maoni

0 Maoni